WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) ametembelea Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nane Nane 2023 yanayofanyika jijini Mbeya, na kujionea shughuli mbalimbali za Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Waziri Mkuu Majaliwa ametumia nafasi hiyo pia kukagua maeneo mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kumpokea Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye atahitimisha kilele hicho Kitaifa tarehe 8 Agosti 2023, jijini Mbeya.
Mheshimiwa Waziri Mkuu katika majumuisho yake ametoa maelekezo kadhaa ikiwemo Mosi, Halmashauri zote nchini kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, kutenga maeneo kwa ajili ya vijana na wanawake ili wakisha pokea mafunzo ya Kilimo Biashara, Uvuvi na Ufugaji waweze kuwa wazalishaji.
Pili, Waziri Mkuu Majaliwa amezitaka taasisi za fedha hususan benki, kuangalia namna ya kushusha riba kutoka asilimia tisa ambayo ni ‘single digit’ hadi kufikia walau asilimia saba
Aidha, Benki ya TADB imetakiwa kufungua matawi zaidi mikoa ya Ruvuma, Iringa na Rukwa na kuacha kutegemea Tawi lake la Mbeya kukidhi huduma za mikoa hiyo, kwani Ukanda huo una Wakulima wengi zaidi.
Tatu, Waziri Mkuu Majaliwa amezitaka halmashauri zote nchini kutenga mapato yanayotokana na kilimo walau Kwa asilimia 20 ili kurejeshwa katika Sekta ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo.
Akiwa kwenye banda la Agricom Waziri Mkuu mbali na kupongeza harakati za kampuni hiyo katika kusaidia maendeleoya kilimo pia ameitaka kuendeleza kampeni yake ya kusaidia vijana na wanawake kufanya kilimo cha kisasa kwa kufikia hadi maeneo ya vijijini
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.