Wanawake wanapaswa kuthaminiwa na kuenziwa kutokana na mchango wao mkubwa katika jamii, ili kuendeleza usawa na maendeleo endelevu.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwa njia ya simu kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Dkt. Ndumbaro alisisitiza umuhimu wa kutambua mchango wa wanawake katika maendeleo ya dunia ya leo.
Akirejea maneno ya msanii Bob Marley katika wimbo wake No Woman No Cry, alieleza kuwa bila mwanamke hakuna mtoto atakayezaliwa, akimaanisha kuwa wanawake wana nafasi muhimu katika uhai wa jamii na ustawi wa dunia.
Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu yanafanyika mkoani Arusha, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.