Waziri wa Afya na Mbunge wa Peramiho , Mheshimiwa Jenista Mhagama, ametangaza rasmi kuwepo kwa ugonjwa wa Mpox (Murbag) nchini Tanzania na kueleza hatua zinazochukuliwa na serikali ili kukabiliana nao.
Akizungumza katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea , Waziri Mhagama amewataka wananchi kupata elimu sahihi kuhusu ugonjwa huo, kujikinga na kuepuka maambukizi.
Ameeleza kuwa Mpox ni ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya kugusana moja kwa moja na mgonjwa, kukumbatiana, kubusiana, pamoja na kutumia vifaa vilivyotumiwa na mtu aliyeambukizwa.
Katika juhudi za kudhibiti ugonjwa huo, Waziri Mhagama amesema kuwa serikali imejipanga kikamilifu na imeandaa kampeni maalum ya siku 54 za mapambano dhidi ya Mpox.
Aidha, ameeleza kuwa mnamo Machi mwaka huu, kulikuwa na tetesi za uwepo wa wagonjwa wenye dalili za Mpox mkoani Kagera, na kufikia Machi 9, 2025, serikali ilithibitisha rasmi kuwa na wagonjwa wawili wa ugonjwa huo.
Amehimiza wananchi kuchukua tahadhari kwa kuzingatia maelekezo ya wataalam wa afya ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.
Mbali na mapambano dhidi ya Mpox, Waziri Mhagama ameweka wazi kuwa serikali inaendelea kufanya juhudi kubwa za kupunguza vifo vya akina mama na watoto.
Amesema kuwa hadi kufikia mwaka 2030, lengo la serikali ni kuhakikisha vifo vya akina mama na watoto vinapungua kwa kiasi kikubwa na kila mama anapata haki yake ya msingi ya kiafya.
Katika hotuba yake, Waziri Mhagama amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake za kuimarisha sekta ya afya
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.