Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi anatarajia kufungua rasmi ofisi ya ardhi ya Mkoa wa Ruvuma katika hafla ambayo itafanyika kwenye viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Agosti 10 mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Ruvuma anamshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa kuwezesha kusogezwa kwa huduma za Wizara ya Ardhi katika ngazi ya Mkoa wa Ruvuma kwa kuanzisha Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Ruvuma.
Amesema wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wameondolewa kero ya muda mrefu kufuata huduma za Wizara ya Ardhi katika Ofisi za iliyokuwa Kanda Mtwara ambapo hivi sasa huduma zote za Kusajili Hati, Kuidhinisha taarifa za Uthamini, Michoro ya upimaji na mipango miji yote yanafanyika katika Ofisi hizi mpya za mkoa wa Ruvuma.
Waziri Lukuvi pia akiwa mjini Songea Agosti 10 mwaka huu anatarajia kuzindua mpango (masterplan) kwa ajili ya kuongoza uendelezaji ardhi ya Manispaa ya Songea baada ya mpango kabambe wa awali kuisha muda wake toka mwaka 2010.Masterplan ya Manispaa ya Songea tayari imeandaliwa na inatumika kuendeleza ardhi ya Manispaa tangu mwaka 2017.
Imeandkiwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.