Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mheshimiwa Innocent Bashungwa anaanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Ruvuma kuanzia Februari 26 hadi 28 mwaka huu.Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo Februari 26 mwaka huu Waziri Bashungwa anatarajia kuanza ziara yake katika wilaya ya Tunduru ambapo atatembelea Makumbusho ya Masonya ambalo ni eneo la urithi wa ukombozi la nyumba ya Samora Machel na Nyerere .
Waziri pia siku ya februari 26 atatembelea wilaya ya Namtumbo kwenye maeneo ya urithi wa ukombozi Likuyu Sekamaganga .ambapo siku ya Februari 27 Waziri wa Habari atahudhuria kilele cha kumbukizi ya miaka 114 ya mashujaa wa Vita ya Majimaji ndani ya viwanja vya Makumbusho ya Taifa ya Majimaji mjini Songea,pia atatembelea Makumbusho ya Kawawa yaliyopo mjini Songea.
Februari 28 Waziri atahitimisha ziara yake kwa kutembelea Barabara ya ukombozi iliyopo kijiji cha Liangueni kata ya Litapwasi Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Februari 26,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.