UKIISHIRIKISHA JAMII KWENYE UTUNZAJI VYANZO VYA MAJI UTAFANIKIWA USIPOISHIRIKISHA UTAKWAMA-WAZIRI WA MAJI
Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso amewataka wakurugenzi wa raslimali za maji na wadau wote wa maji kuhakikisha wanaishirikisha jamii katika utunzaji wa vyanzo vya maji ambavyo vinapatikana katika jamii husika.
Ametoa maagizo hayo hivi karibuni mjini Songea wakati anazungumza na wadau wa maji mkoani Ruvuma katika ziara ya kikazi ya kutembelea Bonde la Maji la ziwa Nyasa ambalo ni bonde la pili kwa kuwa na maji mengi..
Tanzania ina mabonde tisa ya maji ambapo Waziri wa Maji ametembelea mabonde yote tisa kukagua vyanzo vya maji kwenye mabonde hayo na kutoa maagizo ili kuvitunza vyanzo hivyo ambavyo vinaharibiwa kutokana na shughuli za kibinadamu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.