• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WAZIRI wa Maliasili na Utalii azindua chanjo ya UVIKO 19 Kata ya Subira

Imewekwa kuanzia tarehe: November 2nd, 2021

Halmashauri ya Manispaa ya Songea imezindua rasmi miradi ya kuboresha miundombinu ya afya na elimu kwa lengo la kuanza utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu hiyo.

Miradi hiyo ilizinduliwa na Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro iliyofanyika katika kata ya Subira Manispaa ya Songea 31 Oktoba 2021 ambayo ilihusisha ujenzi wa madarasa mawili pamoja na mradi wa maji utakaojengwa katika Kata hiyo pamoja na uwekaji wa jiwe la msingi katika Bwalo la chakula katika Sekondari ya Emanuel Nchimbi.

Dkt. Ndumbaro alisema kuwa fedha hizo zilizotolewa haziwezi kutatua changamoto zote zilizopo na hivyo amewataka wananchi kuchangia nguvu zao ili kuokoa kiasi cha fedha  ili ziweze kuongeza mradi mwingine. Ikumbumbukwe ya kuwa Manispaa ya Songea imepokea fedha million 660,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika Sekondari 26, ujenzi madarasa katika vituo shikizi kwa shule za msingi Nonganonga pamoja na ujenzi wa bwalo la chakula kwa shule yenye wanafunzi wenye mahitaji maalmu katika shule ya Msingi Ruhila.

Aliongeza kuwa Manispaa ya Songea imejipanga kujenga mradi wa gofu ambao utasaidia kujenga hoteli kubwa 5 na kuongeza fursa za ajira kwa vijana pamoja na kuleta maendeleo na kuboreshwa kwa miundombinu ya barabara kama ilivyo kwa mji mitano pekee nchini Tanzania yenye viwanja vya gofu ambayo ni Dar es Salaam, Moshi, Arusha, Morogoro na Mufindi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema ameitaka Halmashauri ya Manispaa ya Songea kusimamia wahandisi wote kwa kuhakikisha wanakuwepo kwenye maeneo ya ujenzi wa miradi  ili waweze kusimamia kwa ufanisi na kwa  uhakika wa ubora wa utekelezaji wa miradi hiyo.

Kamando amesisitiza kuwa miradi hiyo inatakiwa kutekelezwa kwa wakati ambapo hadi kufikia tarehe 15 Disemba 2021 miradi hiyo itakabidhiwa rasmi kwenye tathimini ya Mkoa wa Ruvuma na hivyo wataalamu wahakikishe   wanakuwa makini katika kusimamia  zoezi hilo.

Amewataka viongozi wa Serikali za mitaa kufanya mikutano ya hadhara kwenye maeneo yao ili kuendelea kuhamasisha wananchi kushiriki katika utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuhakikisha maeneo yaliyochaguliwa kujenga miradi hiyo hayabadilishwi.

Nae Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Hamisi Abdallah Ally amewataka wananchi kutoa ushirikiano wakati wa ujenzi wa madarasa hayo ili kufanikisha ujenzi huo.

Akitoa ufafanuzi kuhusiana na kupanda kwa bei ya mbolea alisema kuwa tatizo la kupanda kwa bei ya mbolea imetokana na kufungwa kwa viwanda  vya kuzalisha mbolea kutoka nchi za nje zilizoendelea kutokana na ugonjwa wa UVIKO 19.” alibainisha”

Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa hatari wa UVIKO 19 pamoja na kuendelea kupata chanjo kwa hiari ya ugonjwa huo.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.