• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WAZIRI wa Uchukuzi aridhishwa na upanuzi wa kiwanja cha Ndege Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: July 15th, 2022

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete,amekagua mradi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Songea ambacho Serikali imetoa Sh.bilioni 37.09 kutekeleza mradi huo.

Akizungumza mara baada ya kukagua ukarabati huo,Naibu Waziri  Mwakibete amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo ambazo zinakwenda kuufungua mkoa wa Ruvuma na Tanzania kwa ujumla katika usafiri wa anga.

Naibu Waziri Mwakibete ameridhika  na kazi iliyofanywa na wakala wa Barabara nchini(Tanroads)mkoa wa Ruvuma katika utekelezaji wa mradi huo  muhimu kiuchumi.

Hata hivyo,ameiagiza Tanroads kumsimamia mkandarasi kampuni ya Chico ili kukamilisha kazi  zilizobaki ikiwamo kufunga taa  ili kuruhusu  ndege kutua na kuruka saa 24  badala ya kutumika mchana tu.

Naibu Waziri Mwakibete,ameishauri Tanroads na mamlaka ya viwanja vya ndege(TAA)kuangalia namna ya kuongeza ukubwa wa uwanja huo kwa kuanza mchakato wa kuwalipa fidia baadhi ya wananchi wanaoishi maeneo jirani,hasa upande wa Barabara kuu ya Songea-Mbinga ili kuwezesha ndege kubwa zaidi kama AirBus na Dream liner katika kiwanja hicho.

“nawaomba wenzetu wa Tanroads na mamlaka ya viwanja vya ndege nchini,kwa sasa ndege pekee inayoweza kutua katika uwanja huu ambayo ni kubwa zaidi ni aina ya Bombadier tu,lakini ndege kama AirBus au Dreamliner haziwezi kutua,kwa hiyo ni vyema kuanza mchakato wa kuongeza ukubwa wa  kiwanja chetu”alisema.

Mwakibete alieleza kuwa,mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula,uchimbaji wa makaa ya mawe na kuna ziwa maarufu la nyasa ambapo lengo  kubwa la Serikali ya awamu ya sita kiwanja hicho kitatumika kusafirisha bidhaa  ikiwamo makaa ya mawe.

Aidha,amewataka wakazi wa mkoa wa Ruvuma na mikoa jirani ya nyanda za juu kusini,kuhakikisha wanatumia  fursa ya upanuzi wa kiwanja hicho kuongeza uzalishaji wa bidhaa na kusafiri kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kibiashara na utalii.

Alisema,upanuzi na ukarabati wa kiwanja cha ndege Songea kunatoa fursa za uwekezaji na utalii kwa sababu mkoa wa Ruvuma una vivutio vingi na vya kila aina ikiwamo Ziwa Nyasa,Hifadhi ya Taifa ya Nyerere na maeneo mengi yenye utalii wa kihistoria na kiutamaduni.

Kwa upande wake Meneja wa wakala wa Barabara Tanroads mkoa wa Ruvuma Mhandisi Ephatar  Mlavi alisema, kazi ya upanuzi na ukarabati wa kiwanja cha ndege Songea ilianza 2019 ulitakiwa kukamilika mwezi Disemba 2020.

Hata hivyo alisema,kutokana na kuongezeka kwa baadhi ya kazi walilazimika kuongeza muda hadi tarehe 30 JUNI 2022 na muda wa matazamio ni miezi kumi na mbili.

Alisema, gharama ya mradi ni Sh.bilioni 37.9 na hadi sasa mkandarasi ameshalipwa shilingi bilioni 21.381 na fedha nyingine ambazo ni Sh.bilioni 2.1 zinaendelea kushughulikiwa ili ziweze kulipwa na kazi  hiyo imefikia asilimia 90.

Alisema,kazi zilizofanyika hadi sasa ni ujenzi wa sehemu ya kutua na kurukia ndege,upanuzi wa sehemu ya usalama wa uwanja kila upande,sehemu ya maegesho ya ndege,kuchora mistari na kujenga mifereji yenye urefu wa mita 6000.Aidha alitaja kazi nyingine zilizofanywa na mkandarasi ni kujenga uzio kuzunguka uwanja,kujenga barabara mbili ndani  na nje ya uzio kuzunguka uwanja,kufunga taa za kuongozea ndege ambazo ujenzi wake utakamilika mwishoni mwa mwezi Julai ili kuruhusu ndege kuruka na kutua usiku.

Kwa mujibu wa Mlavi kazi nyingine ni zilizofanyika ni ujenzi wa jengo la kuongozea ndege(Control Tower) ambalo umefikia asilimia 75,ununuzi wa gari la zimamoto lenye uwezo wa kubeba maji lita 10,000 ambalo limeshaagizwa,kujenga jengo la kupokea na kusambaza umeme.

Mlavi alisema,mkandrasi kwa sasa anaendelea kukamilisha kazi ndogo ndogo zilizobaki ambazo zitafanywa  katika muda wa matazamio na atakabidhi kazi zote Mwezi Agosti mwaka huu.

Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Songea Dkt Frederick Sagamiko,ameishukuru Serikali kwa kazi nzuri ya upanuzi wa kiwanja cha ndege Songea na kuhaidi kwamba wananchi wa Songea na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla watahakikisha wanatumia kiwanja hicho  kupanua shughuli za kiuchumi ikiwamo kufanya biashara na kusafirisha bidhaa mbalimbali kwenda mikoa mingine na nje ya nchi.

Dkt Sagamiko ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea alisema,katika mkoa wa Ruvuma kuna fursa nyingi ambazo kupitia kiwanja hicho watabadili mtazamo katika shughuli za kilimo kwa kuanza kulima maua na bustani za mboga mboga ambazo mahitaji yake ni makubwa hapa nchini na nje ya nchi.

Kwa upande wake kaimu meneja wa kiwanja cha Ndege Songea Jafari Mbayo alisema,mara baada ya serikali kufanya ukarabati  na upanuzi wa kiwanja hicho idadi ya abiria wanaotumia usafiri wa ndege imeongezeka  hadi kufikia 72.

Alisema, hali hiyo inaonesha kuwa kuna abiria wengi wanaosafiri  kwa kutumia kiwanja cha ndege cha Songea kutokana na ukweli kwamba usafiri wa ndege ni wa haraka na salama.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.