• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WENGI wajitokeza kujiandikisha Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: October 21st, 2024

WANANCHI  83,692 sawa na asilimia 79.9 wamejiandikisha kwenye Daftari la orodha la wapiga kura katika Halmashauri ya wilaya Songea mkoani Ruvuma hadi tarehe 18 Oktoba.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri  ya wilaya Songea Elizabeth Gumbo alisema,kati yao wanaume 41,016 na wanawake 42,676 huku idadi ya watau ikitarajia kuongozeka siku mbili zilizobaki kabla ya kuhitimishwa kwa zoezi la uandikishaji wapiga kura tarehe 20 mwezi huu.

Amesema,lengo la Halmashauri hiyo ni kuandikisha watu 104,698 wenye umri wa miaka 18 na kuendelea kutokana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022,lakini  idadi hiyo itaongezeka kutokana na uhamasishaji mkubwa unaoendelea katika maeneo mbalimbali.

Gumbo,ametoa wito kwa wananchi ambao bado hawajajiandikisha kwenda kujiandikisha ili kupata haki ya kidemokrasia ya kuchagua viongozi wa vitongoji na vijiji kwenye maeneo yao.

“Katika zoezi hili changamoto kubwa  ni uelewa  wa wananchi kuchanganya uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu,wengi wanategemea kuwa wakijiandikisha watapata vitambulisho vya mpiga kura,napenda kuwafahamisha wananchi kuwa haya ni mazoezi mawili tofauti”alisema Gumbo.

Kwa mujibu wa Gumbo, mwaka 2024 unafanyika uchaguzi wa Serikali za mitaa na katika zoezi hilo Serikali inaandikisha wakazi waliopo kwenye kitongoji husika  hivyo wananchi wanatakiwa wawepo kwenye Daftrai la orodha ya mpiga kura.

Alieleza kuwa,Daftari hilo  litatumika kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa  tu  utakaofanyika tarehe 27 Mwezi ujao na vitambulisho wanavyoulizia vitatolewa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Alisema,wananchi watakojiandikisha katika Daftari la orodha la wapiga kura ndiyo watakaopata fursa ya kupiga kura kwa ajili ya kuchagua viongozi wao katika uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Gumbo,amewataka watendaji wa vijiji na kata kuendelea kuhamasisha wananchi katika maeneo yao ili  waweze kujitokeza kujiandikisha ili kufikisha lengo la kuandikisha wananchi 104,698 katika Halmashauri hiyo.

Katika hatua nyingine,Gumbo amefanya kikao na wadau wa vyama vya siasa kwa lengo la kujadili maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za mitaa ambapo amewataka wadau hao kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa haki,amani na utulivu.

Aidha alisema,idadi ya vitongoji katika Halmashauri hiyo itabaki 443 na mabadiliko  yatakuwa ni kuongezeka kwa vituo vya kujiandikisha na kupiga kura ambavyo vitakuwa 453.

Amesema,lengo la kuongeza vituo hivyo ni kurahisisha huduma kwa wananchi ili wasilamike kutembea umbali mrefu kwenda kwenye vituo vya kupiga kura.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama,amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kwa kazi kubwa anayoifanya kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha katika Daftari la mpiga kura.

Mhagama ambaye ni Waziri wa afya,amewataka wananchi wa jimbo la Peramiho ambao bado hawajajiandikisha kutumia siku chache zilizobaki kwenda kujiandikisha ili waweze kupata fursa ya kuchagua viongozi wao wa vitongoji na vijiji kwenye uchaguzi unaoatarajia kufanyika mwezi ujao.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.