• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WEZI ndani ya magari wanaswa Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: April 24th, 2024


Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumkamata Alpher Christophrer Minja mkazi wa eneo la Sanawali jijini Arusha ambaye alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu kwa makosa ya unyang’anyi na wizi ndani ya magari ambayo yalikuwa yanaegeshwa maeneo mbalimbali ya hoteli,nyumba za kulala wageni na kwenye kumbi za starehe Manispaa ya Songea.

Akizungumza na waandishi wa habari  Kamanda wa Polisi Mkoani Ruvuma Marco Chilya amesema kuwa kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko kuwa watu wakiwa kwenye maeneo hayo wakiwa wameegesha magari yao na kutoka kwenda kwenye hoteli au kumbi za starehe walikuwa kuibiwa mali zao walizokuwa wamezihifadhi kwenye magari yao jambo ambalo lilikuwa kero kubwa kwa wakazi wa Songea.

Amebainisha kuwa Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama walifanikiwa kupata upelelezi wa kina ambao ulisababisha kupatikana kwa mtuhumiwa ambaye alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu na kwamba baada ya mahojiano ya awali na Polisi imebainika kuwa mtuhumiwa Minja alitokea mkoani Arusha na alifika Songea mkoani Ruvuma na kufanya matukio ya unyang’anyi na wizi wa mali za raia ambazo walikuwa wamezihifadhi kwenye magari yao.

Amesema mtuhumiwa Minja baada ya kumuhoji kwa kina zaidi kuhusiana na matukio hayo imebainika kuwa alikuwa na wenzake watatu ambao majina yao yamehifadhiwa kwa upelelezi zaidi wanaodaiwa kuwa walikuwa wakisaidiana na Minja kufanya uhalifu kwenye maeneo ya kumbi za starehe, Hoteli, nyumba za kulala wageni na baa mjini Songea.

Kwa mujibu wa Chilya Minja amekamatwa kwa makosa ya unyang’ anyi na wizi ndani ya magari yaliyo kuwa yameegeshwa kwenye maeneo mbalimbali akiwa na jumla ya Laptop 10 mali ambazo zilikuwa zimeibiwa maeneo tofauti mjini Songea na kwamba mtuhumiwa Minja anatarajiwa kufikishwa mahakamani yeye pamoja na watuhumiwa wenzake watatu mara tu baada ya upelelezi kukamilika.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.