Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo,wameandaa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kimkoa inafanyika katika manispaa ya Songea,
Kaulimbiu ya mwaka huu ni wanawake na wasichana 2025 tuimarishe haki,uswa na uwezeshaji
Kwa hiyo kuelekea maadhimisho hayo,ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya songea wameandaa shughuli mbalimbali katika wiki ya maadhimisho na siku ya kilele tarehe 8 Machi,2025.
Shughuli zilizopangwa kufanyika ni Pamoja na kongamano la wanawake ambalo limepangwa kufanyika Machi 3 kwenye kwenye ukumbi wa Parokia ya Bombambili Songea kuanzia saa tatu asubuhi.
Machi 4,2025 kwenda kutembelea watu wahitaji wenye ukoma na Watoto wenye usonji katika Kijiji cha Morogoro
Machi 6,2025 kutakuwa na uzinduzi wa maadhimisho na maonesho katika viwanja vya soko kuu Songea kuanzia saa 3 asubuhi.
Kilele cha maadhimisho ni tarehe 8/3/2025 katika uwanja wa Majimaji Songea kuanzia saa mbili asubuhi.
Machi 9,2025 kutakuwa na usiku wa mwanamke kuanzia saa 12;00 jioni kwenye ukumbi wa Parokia ya Bombambili Songea
Aidha kuna sare ya kitenge ya siku ya kilele cha maadhimisho ya wanawake inayopatikana katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa shilingi 26,000.
Tiketi za usiku wa mwanamke zinapatikana kwa shilingi 50,000 VIP na shilingi 30,000 kadi za kawaida ambazo zinapatikana ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Wanawake wote wa Mkoa wa Ruvuma mnakaribishwa katika maadhimisho hayo siku ya wanawake Duniani katika uwanja wa Majimaji Songea.
Imetolewa na Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Ruvuma Xsaveria Mlimila
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.