• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WILAYA ya Nyasa yapata mradi wa maji wa bilioni nne

Imewekwa kuanzia tarehe: September 8th, 2023

Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Nyasa  imetambulisha mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya zaidi ya  shilini Bilioni 4.1utakaotatua kero ya  maji safi na Salama katika Kata mbili  za Kilosa na Mbamba bay Wilayani Nyasa.

Mradi huo  umetambulishwa katika mikutano ya Hadhara wenye lengo la kuwashirikisha  wananchi, ili waweze kushirikiana na Mkandarasi atakayetekeleza Mradi, Mkutano  iliyofanyika katika Kata ya Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji Cha Nangombo Kata ya Kilosa  na kuhudhuriwa na wananchi na Viongozi wa Chama na Serikali.

Akizungumza katika Mkutano, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh.Filberto Sanga, amemtaka Mkandarasi anayetekeleza Mradi, kuhakikisha anajenga mradi kwa ubora na kwa wakati na kuhakikisha maji yanatoka, na kuwa Mradi endelevu kwa kuwa Serikali inalengo la kutatua kero ya maji, hivyo fedha za Serikali ziendane na thamani halisi ya Mradi. Pia amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika Mradi na kulinda na kutunza Vyanzo vya maji.

“Ninakutaka Mkandarasi utakayetekeleza Mradi huu kuhakikisha kuwa unajenga kwa ubora na maji yanatoka, na kuwa mradi endelevu  kwa kuwa Serikali inalenga  kutatua kero ya maji, hivyo fedha za Serikali ziendane na thamani halisi ya Mradi,na wananchi naomba tushiriki kikamilifu Ujenzi wa mradi huu Kwa kuwa ni wetu na unalengo la kutatua kero ya maji katika mji wetu wa Mbamba bay Kwa kuwa tulikuwa na miradi midogo midogo

Awali akitoa Taarifa ya Miradi hiyo  Meneja wa RUWASA Wilayani Nyasa mhandisi Masoud Samila,amemtambulisha Mkandarasi Peritus Exim Private ltd kutoka Dar es salaam ndie atakayetekeleza mradi huu na amesema,wamejipanga kimkakati kusimamia na  kutekeleza miradi hiyo ili iweze kutatua  changamoto ya upatikanaji wa maji safi kwa wananchi.

Amesema Mradi huu unalenga kuhudumia wananchi wapatao 13,323 na amevitaja  vijiji vitakavyonufaika na mradi  huu ni Nangombo, Likwilu, Ruhekei, kilosa na Mbamba bay.

Ameongeza kuwa shughuli zitakazofanyika ni Ujenzi wa Tego la maji,ujenzi wa Tanki lenye ujazo wa Lita milioni Moja(1,000,000),ununuzi wa Bomba, ulazaji wa mabomba km 4.9 ujenzi wa vituo 10 vya kuchotea  maji na Miradi hiyo itatekelezwa kwa kipindi cha miezi sita na unatarajia kukamilika January 2024.

Ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na Mkandarasi anayetekeleza mradi huu kwa kuwa anaanza mara moja baada ya kutambulishwa.

Wananchi wa Kata Hizo wameipongeza Serikali kwa, kutatua changamoto ya maji katika kata zao kwa kuwa awali walikuwa na Miradi ambayo ilijengwa zamani na miundombinu yake ilikuwa imechakaa, hivyo wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa Bw Khalid Khalif kwa kutatua Changamoto mbalimbali katika Wilaya ya Nyasa.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.