Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, tarehe 14/02/2023 limepitisha Bajeti ya yenye thamani ya shilingi bilioni 27,653,395,441.07, kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya Halmashauri, katika kikao kilichofanyika , Ukumbi Kepten John Komba Uliopo Mbamba bay Wilayani Nyasa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Bw. Stewart Nombo, ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la Madiwani amesema kuwa baraza limeidhinisha mpango na bajeti ya maendeleo, kwa mwaka wa fedha 2023/2024, kwa kuwa bajeti hii imelenga kutatua kero mbalimbali za wananchi, ikiwa ni pamoja na kutekeleza Miradi ya Maendeleo, na kutoa wito kwa madiwani kutoa ushirikiano kwa wataalamu katika usimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Kata zao.
Akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2023/ 2024, Kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji Wilaya ya Nyasa, Mkuu wa Divisheni ya Mipango na uratibu Bw. Chrstopher Ngonyani amesema, kuwa bajeti hiyo, inalenga
Program mbalimbali zilizopangwa kufanyika katika Halmashauri. Kati ya Kiasi hiki Tsh 16,000,575,951.07 ni matumizi ya kawaida,Tsh 15,196,594951.07 ni mishahara na Tsh 803,981,000.00 ni matumizi mengineyo (OC)Tss 10,068,182,000.00 ni matumizi ya miradi ya maendeleo (Tsh 4,110,371,000.00 ni fedha za ndani na Tsh 5,957,811,000.00 ni fedha za nje na Tsh 1,447,627,190,000.00 ni fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri, kati ya fedha hizo tsh 994,923,000 ni mapato halisi(proper Own Source Tsh 452,704,190.00 ni mapato lindwa na michango ya nguvu ya jamii ni tsh 137,000,000.00.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Bw Jimson Mhagama, amewataka madiwani wa Wilaya ya Nyasa kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao, kwa kushirikiana na wananchi, kutekeleza miradi hiyo na kusema kuwa Miradi hii inatekelezwa kwa fedha za walipa kodi, kwa hiyo ni jukumu la kila kiongozi kusimamia fedha hizo ili kujiletea maendeleo.
“waheshimiwa madiwani ninawataarifu kuwa kila ninapokuandikia na kukupa taarifa za kukuletea fedha katika eneo lako, ni jukumu lako kusimamia, kuwashirikisha wananchi, na kutekeleza miradi kwa ubora wa hali ya juu, kwa kuwa fedha zinazotekeleza miradi hii ni kodi za wananchi wetu na Mh Rais amezileta ili zitatue changamoto za wananchi hivyo kila kiongozi anatakiwa kuwajibika kwa nafasi yake” .
Naye Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya, amesema Wilaya ya Nyasa inakusudia kujenga uwanja wa kisasa mkubwa wa michezo ili kuongeza utalii na kuhamasisha michezo .
Aidha amepongeza Mkurugenzi wa Mtendaji wa Wilaya ya Nyasa Bw Jimson Mhagama, na Wataalamu wake, walioshiriki kuandaa mpango na bajeti ambayo imezingatia vigezo muhimu vyenye lengo la kutatua Kero za wananchi Wilayani Hapa
Naye Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh.Filbetho sanga alijitambulisha katika baraza hilo na kuwaeleza kuwa ameanza kazi katika Wilaya ya Nyasa na ameagiza Uwepo wa ulinzi na Usalama na kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wanaripoti haraka kwa asilimia 100.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.