SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, imetoa mafunzo ya kuzuia na kupambana na magonjwa ya Mlipuko kwa wadau mbalimbali wa maendeleo Wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.
Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Bay live mjini MBAMBA BAY yakihusisha viongozi,, wazee mashuhuri,waganga wa kienyeji na watendaji wa Kata na vijiji na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya redio za kijamii na mitandao ya kijamii..
Mratibu wa mafunzo hayo Johnson Mndeme kutoka Wizara ya Afya amesema lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu Kwa makundi mbalimbali ya kijamii, ili kujenga uelewa wa magonjwa ya Mlipuko na jinsi ya kukabiliana nayo, ili jamii iweze kujua kuzuia na kupambana pindi yanapotokea.
Mndeme amefafanua kuwa Wilaya ya Nyasa Ina mwingiliano kutoka nchi Moja kwenda nyingine hivyo wizara imeona ni vema ikatoa elimu hiyo Kwa makundi mbalimbali ya jamii,ya Nyasa ili iweze kutoa elimu hiyo Kwa wananchi wa Wilaya ya Nyasa.
.Ametoa wito Kwa wananchi wa Wilaya ya Nyasa kutumia vyoo Bora na kunawa maji Kwa usahihi baada ya kutoka chooni na kuchemsha maji ya kunywa.
Akifungua Mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Nyasa Ndugu Bernard Semwaiko amewataka Viongozi wa dini kutoa elimu Kwa waumini wao ili kuzuia na kupambana na magonjwa ya Mlipuko hasa kipindupindu Kwa Wilaya ya Nyasa na kumwambia Nyasa bila kipindupindu Inawezekana.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.