Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amebainisha kuwa Wizara ya Kilimo imekuwa msaada mkubwa kwa Mkoa wa Ruvuma hasa katika kipindi hiki cha uuzaji wa Mahindi.
Ameyasema hayo alipokutana na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe, Waziri wa Maji Juma Awesu na Naibu waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa Katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Amebainisha kuwa Mkoa unakubaliana na viwango vya kusafisha mahindi vilivyowekwa kwa kuwa hauwezi kupata Soko la mazao nje ya Nchi kama mazao hayo yana uchafu.
Ameshauri kuendelea kuwaelimisha Wakulima na NFRA kujumuisha bei ya kilo ya Mahindi na gharama za kusafisha Mahindi ili NFRA iendelee na Jukumu la kusafisha Mahindi na Wananchi waruhusiwe kupeleka Mahindi Yao.
Ameeleza kuwa zipo mashine mahususi za kusafisha Mahindi katika Masoko ya Dunia na kuomba kupatikana kwa mashine hizo kwa msaada wa ubia wa Serikali na wawekezaji ili kuwarahisishia wakulima kusafisha Mahindi Yao.
Ameeleza ipo changamoto ya kukosekana kwa maghala ya kutosha ya kuhifadhia Mahindi na uchache wa magari ya kusafirishia Mahindi kupeleka sehemu za kuhifadhia jambo ambalo Mkoa unaendelea kulitatua.
Ameeleza suala la uuzaji wa mazao kupitia mfumo wa Stakabadhi za ghala ambapo Wizara ya kilimo inaendelea kuunga mkono, na ameshauri kuendelea kusimamia vizuri mfumo huu kwa kuzingatia manufaa ya wakulima.
Kwa Upande wa Waziri wa Maji Juma Awesu, Mkuu wa Mkoa ameeleza wameendelea kushirikiana nae kuhusu maendeleo ya Maji katika Mkoa na Nchi kwa ujumla.
Sanjari na hayo Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa kama Mkoa umejipanga vyema katika kufanikisha shughuli za Tamasha la Utamaduni na Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.