MKUU wa wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Mheshimiwa Ngollo Malenya amekabidhi vifaa vyenye thamani ya milioni 17,850,000 kutoka wizara ya kilimo Kwa maafisa ugani 38 wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo.
Akikabidhi vifaa hivyo Malenya alisisitiza utunzaji wa vifaa hivyo pamoja na wataalamu kuwasaidia wakulima Ili waweze kuzalisha mazao Kwa wingi na Kwa ubora.
Aidha mkuu wa wilaya huyo alidai wilaya ya Namtumbo ni wilaya ya kilimo inayochangia hifadhi ya chakula katika ghala la taifa hivyo aliwaagiza wataalamu kutumia vifaa hivyo kuwaongezea wakulima utaalamu Ili waweze kuzalisha zaidi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Chiriku Hamis Chilumba aliishukuru Serikali Kwa kuwapatia vifaa hivyo Kwa wataalamu wao wa ugani Ili waweze kuwasaidia wakulima utaalamu wa kuzalisha zaidi kupitia kuwahudumia wakulima Kwa ukaribu na kubainisha aina ya udongo unaofaa Kwa kilimo kulingana zao linalohitajika.
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Andrew Tarimo alisema vifaa vilivyopokelewa ni Gumbut ,Bomba za kupulizia wadudu, Makoti ya mvua (Rain coat) pamoja na kifaa Kwa ajili ya kupimia afya ya udongo.
Afisa ugani kasto Ngonyani wa Kijiji Cha mtonya Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo alidai kutolewa Kwa vifaa hivyo vitawarahisishia maafisa ugani kuwaelimisha wakulima kilimo Bora chenye tija Kwa kulima na kuzalisha mazao kulingana na udongo wa eneo husika kutokana na uwepo wa kifaa Cha kupimia afya ya udongo alisema Gambi.
Wilaya ya Namtumbo ni wilaya ya wakulima hivyo kutolewa Kwa vifaa hivyo vitasaidia wataalamu wa ugani waliopo katika Halmashauri ya Namtumbo Kuwaelimisha wakulima kujua aina ya udongo na mazao Gani yanayopaswa kulima kulingana na afya ya udongo uliopimwa Ili wakulima wapate tija katika uzalishaji na kuwaletea wananchi hao Maendeleo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.