• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

WIZARA ya Nishati yakabidhi gari la kubebea nguzo za umeme Mbinga

Imewekwa kuanzia tarehe: July 21st, 2024

Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga leo Julai 20, 2024 amekabidhi gari la kubebea nguzo katika Ofisi ya TANESCO Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma. 

Wakati akikabidhi gari hilo Mhe. Kapinga amesema Serikali itaendelea kuboresha  maslahi, vitendea kazi na mazingira ya kazi kwa Wafanyakazi wa TANESCO ili kuwapa motisha ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii.

"Kulikuwa na changamoto ya kubeba nguzo kupeleka kwenye maeneo mnayofanyia kazi, Serikali inaamini magari haya yataleta tija na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi ikiwemo kutoa huduma kwa wakati kwa wateja." Amesema Kapinga

Akizungumzia  changamoto ya kukatika kwa umeme wilayani Mbinga,  Kapinga amesema Serikali imeshaweka mikakati ya kujenga kituo kipya  cha umeme ambacho kitaboresha hali ya upatikaji umeme.

Ameongeza kuwa,  kituo hicho cha kupokea na kupoza umeme  kitajengwa katika mradi wa Gridi Imara Awamu ya Pili.

Amesema TANESCO inaendelea kuboresha miundombinu ya umeme wilayani humo  wakati ujenzi wa kituo cha kupokea na kusambaza umeme ukisubiriwa.

Katika hatua nyingine, Mhe.Kapinga amewahakikishia wananchi kuwa, Wizara ya Nishati chini ya uongozi wa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, itaendelea kuboresha  utoaji wa huduma na upatikanaji wa nishati ya umeme nchini.

Awali, Meneja wa TANESCO  Wilaya ya Mbinga, Mhandisi Edward Kweka alisema kuwa walikuwa wakikutana na changamoto ya ubebaji nguzo kutokana na kutokuwepo kwa gari la kubebea nguzo hizo..

Mhandisi Kweka amesema gari hilo litawasaidia kutoa huduma kwa ufanisi na kuahidi kulitunza.

TANESCO Wilaya ya Mbinga inajumla ya wateja 37,925 na inapokea umeme wa gridi ya Taifa wa kilovoti 33 kutoka kituo cha kupoza umeme cha Songea.


Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.