MAKUMBUSHO ya Taifa ya Majimaji yaliyopo Mahenge mjini Songea,ni miongoni mwa makumbusho saba ya Shirika la Makumbusho ya Taifa na vituo 91 vya kale vilivyopo nchini.
Makumbusho ya Majimaji yalianzishwa na kufunguliwa Julai 6,1980,lengo la kuanzisha makumbusho hayo ni kutunza kumbukumbu ya historia ya vita ya Majimaji iliyoanza mwaka 1905 hadi 1907.
Mhifadhi wa Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Adson Ndyanabo anasema Makumbusho hiyo imejengwa katika eneo eneo ambalo mashujaa 67 walizikwa baada ya kunyongwa kikatili na wajerumani.
Analitaja eneo hilo la mashujaa maarufu kama hero square kuna makaburi mawili ya mashujaa moja ni la halaiki ambalo wamezikwa mashujaa 66 katika kaburi moja baada ya kunyongwa na serikali ya wakoloni wa kijerumani Februari 27,1906.
Kwa mujibu wa Mhifadhi huyo,kaburi la pili lililopo kwenye makumbusho hayo ni la Jemedari wa wangoni,Nduna (Sub chief) Songea Mbano aliyenyongwa Machi 2,1906.Mji wa Songea umepewa jina la jemedari huyo.
Licha ya uwepo wa Makumbusho ya Taifa ya Majimaji,Mhifadhi huyo anasema katika mji wa Songea kuna Makumbusho ya Dkt.Rashid Mfaume Kawawa.
Anasema katika maadhimisho ya kumbikizi ya mashujaa wa vita ya Majimaji yaliyofanyika Februari 27,2015,sanjari na onesho la Historia ya Hayati Dkt.Rashid Mfaume Kawawa,familia iliahidi kutoa nyumba moja kubwa ya mbele ya familia na nyumba nyingine za uwani zilizopo katika eneo la Bombambili mjini Songea kwa Makumbusho ya Taifa ya majimaji.
Analitaja lengo kuu la kuanzisha makumbusho hayo kuwa ni kutunza na kuhuisha historia nzuri ya kutukuka ya hayati Dkt.Rashid Mfaume Kawawa(Simba wa Vita).
Kulingana na Mhifadhi huyo,Makumbusho ya Dkt.Rashid Kawawa yalianzishwa na kufunguliwa rasmi februari 27,2017 ambapo hivi sasa ukarabati unaendelea chini ya Wakala wa Majengo Tanzania(TBA) Mkoa wa Ruvuma.
Anasema serikali ya Awamu ya Tano imetoa zaidi ya shilingi milioni 164 kwa ajili ya ukarabati wa Makumbusho ya Dkt.Rashid Mfaume Kawawa,kazi ya uboreshaji ambayo inasimamiwa na TBA bado inaendelea.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.