MKUU wa mkoa wa Ruvuma Brigadia Jenerali Wilbert Ibuge, amewataka viongozi wa Dini mkoani humo, kuchukua tahadhari wakati wa ibada kwa kuvaa Barakoa na kunawa mikono wakati wote wa ibada ili kujinga na ugonjwa wa Corana.
Jenerali Ibuge ametoa kauli hiyo alipokutana na Askofu wa Kanisa Katolki Jimbo la Tunduru- Masasi Mhashamu Filbert Mhasi, kwa ajili ya kumpa pole kufuatia kifo cha Naibu Askofu wa Jimbo hilo Marehemu Castor Msemwa aliyefariki mwaka 2018.
Aidha amewaomba viongozi hao kusaidiana na Serikali kutoa elimu juu ya ugonjwa huo kwa wananchi na waumini wao, badala ya kazi hiyo kuiachia Serikali hasa ikizingatia kuwa viongozi wa Dini wana nafasi kubwa ya kukutana na kufikisha elimu kwa jamii kwa haraka.
Amesema, anatambua juhudi mbalimbali zinazofanywa na viongozi wa Dini katika wilaya hiyo na mkoa wa Ruvuma kwenye mambo mbalimbali ya imani na maendeleo,hata hivyo bado wana wajibu wa kuendelea kuelimisha jamii kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo.
Aidha Jenerali Ibuge,amewaomba viongozi wa madhehebu ya Dini kuendelea kushikamana na kutoa elimu kwa wananchi wetu kuhusu tishio la ugaidi lililoanza kujitokeza katika mpaka wetu na Nchi jirani ya Msumbiji.
Amesema,suala la ulinzi wa mipaka yetu ni la kila mtu, kwa hiyo kama tukilegea kidogo inaweza kuathiri hata kwetu hivyo amesisitiza ni lazima tuzuie tishio la aina yoyote na kuhakikisha usalama wa nchi yetu unadumishwa ili kutoa nafasi kwa wananchi kuendelea kufanya shughuli zao za maendeleo.Amewataka viongozi wa Dini, kuwaelimisha wananchi kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama pale wanapoona kuna dalili za mtu au kikundi cha watu wasioeleweka katika maeneo yao kwani Serikali haiwezi kuweka wanajeshi kila mahala, lakini wananchi kama watatoa taarifa mapema itasaidia sana kuchukua hatua dhidi ya matukio ya aina hiyo.
Pia Jenerali Ibuge, amelishukuru Kanisa Katoriki Jimbo la Tunduru-Masasi kwa namna ambavyo limeendelea kutoa huduma mbalimbali kwa jamii kitu ambacho kina tija na ustawi mkubwa kwa wananchi na Nchi kwa jumla.
Amesema, mara nyingi binadamu wana tabia ya kusifia vitu baada ya kupita na ndiyo wanavikumbuka,lakini ni vyema kutiana moyo na kutambua jitihada ambazo zinazofanyika na Kanisa Katoriki za kuunga mkono juhudi za Serikali za kuwaletea wananchi maendeleo.Kwa upande wake Askofu wa Kanisa hilo Filbert Mhasi, ameishukuru Serikali ya wilaya na mkoa kwa kuwa bega kwa bega na kanisa hilo wakati wote wa msiba wa Askofu Msemwa na wakati wa kusimikwa kwake kuwa Askafu wa Jimbo hilo mwaka 2019.
Amesema, yeye kama kiongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Tunduru-Masasi ataendelea kushirikiana na serikali katika shughuli zote za maendeleo kwa ajili ya ustawi wa waumini,wananchi na Taifa.
Amesema,anatambua kazi kubwa inayofanywa na viongozi wa Serikali za kuleta maendeleo kwani kwa muda mfupi amewaona jinsi wanavyoangaika kuhusiana na suala la elimu katika jamii ya wana Tunduru ambayo bado iko nyuma sana hususani kwa watu wa kike.
Amesema, kwa nyakati tofauti viongozi wa Serikali wakiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Julius Mtatiro wanapita vijijini na wakati mwingine kulazimika kwenda hadi mstuni kuwasaka watoto waliacha shule ili waweze kuendelea na masomo. TAZAMA HABARI KWA KINA HAPAhttps://www.youtube.com/watch?v=ieiIHbnOAzI
ReplyForward |
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.