• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

ZAIDI ya bilioni 5.799 kutekeleza miradi nane ya maji Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: January 14th, 2021

WILAYA ya Songea  mkoani Ruvuma inatarajia kutumia zaidi ya shilingi bilioni 5.799 kutekeleza miradi nane ya maji katika kipindi cha mwaka 2020/2021.

Meneja  Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA)  Wilaya ya Songea Mhandisi Mathias Charles amesema hadi kufikia Januari mwaka huu RUWASA Wilaya ya Songea imepokea zaidi ya shilingi milioni 877 sawa na asilimia 15.12 ya bajeti iliyopangwa.

“Hadi kufikia Januari 2021 wakazi wanaopata huduma ya maji wilaya ya Songea wanakadiriwa kuwa 132,362 sawa na asilimia 63.6 ya wakazi wote’’,alisema Charles.

Hata hivyo amesema hadi sasa Mamlaka hiyo imetumia zaidi ya shilingi bilioni tatu kutekeleza miradi tisa ya maji  katika wilaya hiyo na kwamba RUWASA  inaendelea na kazi ya uboreshaji wa huduma ya upatikanaji wa maji kwa kujenga miradi mipya.

Kulingana na Meneja huyo,RUWASA inaendelea kukarabati miradi iliyokuwa imechakaa na kuboresha usimamizi wa miradi ya maji iliyokamilika ili iwe endelevu kwa kuunda na kusajili Jumuiya za watumiaji maji(CBWSOs) ambazo zitakuwa zinasimamia miradi hiyo na kuhakikisha inatoa huduma wakati wote.

Amesema katika kipindi cha mwaka 2019/2020 RUWASA Wilaya ya Songea  ilipanga kuunda na kusajili jumuiya za watumiaji maji 17 ambapo hadi kufikia Juni 2020 jumuiya 10 zilikuwa zimeundwa na kusajiliwa.

Hata hivyo amesema kwa mwaka wa fedha 2020/2021 jumuiya za watumiaji 28 zilipangwa kuundwa na kusajiliwa ambapo hadi kufikia Januari 2021 jumuiya 11 zimeundwa.

Ameitaja miradi ya maji iliyopangwa kutekelezwa katika Halmashauri ya Madaba kupitia P4R kuwa ni Ndelenyuma,Lutukira na Mbangamawe ,kupitia PBR4 mradi mmoja wa maji katika kijiji cha Igawisenga unatarajia kutekelezwa.

Kwa mujibu wa Meneja huyo wa RUWASA,katika Halmashauri ya Songea vijijini kupitia P4R miradi ya maji inatarajia kutekelezwa katika vijiji vya Lipaya,Lundusi na Maposeni,kupitia PBR4 mradi mmoja wa maji unatarajia kutekelezwa katika kijiji cha Ndongosi na mradi mmoja unatarajia kutekelezwa Ndilimalitembo Manispaa ya Songea.

Amesema RUWASA Wilaya ya Songea imepanga kukamilisha zoezi la usajili Jumjuiya za watumiaji maji ifikapo Juni 30 mwaka huu na kwamba RUWASA  imejipanga kuendelea kutoa elimu juu ya utunzaji vyanzo vya maji na elimu kuhusu umuhimu wa ulipaji wa huduma ya maji ili kuifanya miradi iwe endelevu.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Januari 14,2021

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

    June 01, 2025
  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.