KILO milioni 19,375,896.00 za korosho zenye thamani ya Sh.bilioni 62,159,126,758.00 zimeuzwa na wakulima wanaohudumiwa na Chama kikuu cha Ushirika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma(TAMCU Ltd).
Korosho hizo zimeuzwa katika minada minne kupitia mfumo wa stakabidhi ghalani chini ya usimamizi wa mfumo soko la bidhaa(TMX) ulioonyesha mafanikio makubwa kwa wakulima kupata soko la uhakika na bei nzuri ya zao hilo.
Meneja Mkuu wa TAMCU Marcelino Mrope alisema,mnada wa kwanza ulifanyika katika kijiji cha Nakapanya kilo 1,804,369.00 zenye thamani ya Sh.5,792,024,490.00 zimeuzwa kwa bei ya Sh. 3,210 kwa kilo moja.
Mrope alisema,katika mnada wa pili uliofanyika katika kijiji cha Mtina wakulima wameuza kilo 7,543,517.00 zenye thamani ya Sh.23,973,297,026.00 kwa bei ya Sh. 3,178.
Kwa mujibu wa Mrope,mnada wa tatu uliofanyika kijiji cha Airpot kata ya Mbesa, kilo 5,190,191.00 zimeuzwa kwa bei ya Sh.3,212 huku wakulima wakipata zaidi ya Sh. 16,670,893,492.00 na katika mnada wanne uliofanyika tarehe 12 Novemba kijiji cha Ligoma kilo 4,837,819.00 zenye thamani ya Sh.15,722,911,750.00 ziliuzwa kwa bei ya Sh.3,250.
Alieleza kuwa,katika mchakato wa mauzo ya korosho hadi sasa hakuna usumbufu wowote na wakulima wanapata fedha zao kwa wakati, na wanunuzi wanafanya malipo kupitia Chama kikuu cha Ushirika tofauti na hapo awali ambapo malipo yalipitia kwenye Amcos.
Mrope,amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo yake kutaka malipo ya wakulima yanafanyika kupitia chama kikuu kwani yamerahisisha sana ulipaji fedha za wakulima kutoka siku 14 hadi siku 4 tangu mnada unapofanyika.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.