• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

ZIWA Nyasa kutumika kama Ziwa Viktoria

Imewekwa kuanzia tarehe: November 28th, 2022

ZIWA NYASA KUTUMIKA KAMA ZIWA VIKTORIA 

MKURUGENZI Mkuu wa RUWASA nchini Mhandisi Clement Kivegalo amesema yeye ndiye aliyesimamia mradi mkubwa wa maji kuyatoa ziwa Viktoria na kuyapeleka kwenye mikoa yenye uhaba wa maji

Amesema  mradi kama huo unaweza kufanyika katika ziwa Nyasa na kupunguza uhaba wa maji nchini.

Mhandisi Kivegalo amesema hayo wakati anazungumza baada ya kukagua mradi mkubwa wa maji wa Mwerampya Kata ya Lituhi Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni 6.4.

“Mimi ndiye nilisimamia mradi wa kuyatoa maji Ziwa Viktoria kuyapeleka Shinyanga,Kahama,na sasa yamefika Tabora,Igunga,Nzega na Sheluwi na yataenda Sikonge,Urambo na Kariua”,alisema.

Mhandisi Kivegalo amesema maji haya yametoka kwenye plant moja hivyo serikali inaweza kutekeleza mradi kama huu kwenye Ziwa Nyasa.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya ameipongeza RUWASA kwa kutekeleza miradi mikubwa miwili ya maji katika Kata za Lituhi na Liuli yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 11 .

Amesema miradi hiyo ambayo inatarajia kukamilika Aprili 2023 inakwenda kumaliza changamoto ya maji katika vijiji 13 vilivyopo kwenye mradi.

Hata hivyo amesema Wilaya ya Nyasa ina vyanzo vingi vya maji likiwemo Ziwa Nyasa ambalo linaweza kumaliza changamoto ya maji katika Mkoa wa Ruvuma na mikoa jirani.

Mhandisi Manyanya anaunga mkono wazo la kutekeleza mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Nyasa na kuyapeleka maji hayo katika maeneo mengine yenye uhaba wa maji nchini.

Ziwa Nyasa ni miongoni mwa maziwa makubwa matatu  nchini,Ziwa hili linatumiwa na nchi tatu za Tanzania,Malawi na Msumbiji.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma 

Novemba 28,2022

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.