Mkoa wa Ruvuma unazalisha zao la Samaki katika Ziwa Nyasa wastani wa tani 8,411.4 kwa mwaka sawa na thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 25.
Hayo amesema afisa uvuvi Mkoa wa Ruvuma Amuli Bazili ofisini kwake kuwa Mkoa unategemea kupata Samaki kutoka Ziwa Nyasa mito,Mabwawa ya asili na mabwawa ya kufugia Samaki.
Hata hivyo Bazil amesema tija inayopatikana na vyanzo vya Samaki haitoshelezi mahitaji ya Mkoa ambayo ni zaidi ya tani 18,000 kwa Mwaka na kupata samaki kutoka nje ya Mkoa wastani wa Tani 55 kwa mwezi.
Amesema kwa kipindi cha mwaka 2021 /2022 wavuvi walisajiliwa pamoja na vikundi 38 vya wavuvi na vikundi vinne vya ulinzi wa rasilimimali za uvuvi vilivyopo katika mialo ya Mbamba bay,Lituhi,Ndengele na Ng’ombo.
“Mkoa una jumla ya wafugaji wa samaki 4,170 wenye jumla ya mabwawa 6,602 yenye wastani wa uzalishaji wa tani 847.9 kwa mwaka”.
Hata hivyo amesema ufugaji wa Samaki ni shughuli ambayo wananchi wengi wamekuwa wakifanya katika kuongeza kipato na lishe katika jamii inayowazunguka kutokana na kutotosheleza kwa samaki wanaotoka kwenye vyanzo vya samaki vilivyopo kwenye Mkoa.
Afisa uvuvi ametoa rai kwa kuwahamasisha wananchi kwa kuendelea kufuga samaki kwa tija katika mabwawa ili kuweza kukidhi mahitaji kwaajili ya chakula na biashara.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Octoba 13,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.