5.2.5 Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo katika utekelezaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa ya kidato cha kwanza 2023.
Mkoa wa Ruvuma ulipokea fedha nje ya bajeti TShs.3,120,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 156 vya kidato cha kwanza 2023 katika shule za sekondari. Mchanganuo wa Fedha hizo ni kama inavyoonesha kwenye jedwali namba 7.
Jedwali Na. 7: Mchanganuo wa Fedha za Mpango wa Maendeleo kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya kidato cha kwanza 2023.
HALMASHAURI
|
IDADI YA VYUMBA VYA MADARASA
|
MGAO WA FEDHA
|
VILIVYOKAMILIKA
|
HATUA YA UKAMILISHAJI
|
ASILIMIA
|
TUNDURU DC
|
10 |
200,000,000.00 |
10 |
0 |
100 |
MBINGA DC
|
10 |
200,000,000.00 |
0 |
10 |
0 |
MBINGA TC
|
11 |
220,000,000.00 |
6 |
5 |
52 |
NAMTUMBO DC
|
17 |
340,000,000.00 |
3 |
14 |
17.6 |
SONGEA DC
|
10 |
200,000,000.00 |
7 |
3 |
95 |
MADABA DC
|
10 |
200,000,000.00 |
1 |
9 |
10 |
NYASA DC
|
12 |
240,000,000.00 |
8 |
4 |
67 |
SONGEA MC
|
76 |
1,520,000,000.00 |
0 |
76 |
0 |
JUMLA
|
156 |
3,120,000,000.00
|
35 |
121 |
22.4 |
Hadi kufikia tarehe 30 Novemba, 2022 jumla ya vyumba 35 vya madarasa vimekamilika sawa na asilimia 22.4 na vyumba 121 vipo hatua za ukamilishaji.
5.2.6 Mapokezi ya fedha za ujenzi wa vituo vya afya na nyumba za watumishi kwa halmashauri
Mkoa umepokea jumla ya TShs. 980,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya vitatu na nyumba nne za watumishi wa halmashauri. Fedha hizi zimetokana na ruzuku ya serikali kuu na mapato ya ndani ya Halmashauri ikiwa ni jitihada za kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma bora karibu na maeneo yao. Mchanganuo wa fedha ni kama inavyonesha kwenye jedwali namba 8.
Jedwali Na 8. Mapokezi ya Fedha za Ujenzi wa Vituo vya Afya na nyumba za watumishi wa halmashauri
HALMASHAURI
|
IDADI VITUO VYA AFYA
|
KIASI CHA FEDHA KWA VITUO VYA AFYA
|
IDADI YA NYUMBA ZA WATUMISHI
|
KIASI CHA FEDHA NYUMBA ZA WATUMISHI
|
SONGEA MC
|
0 |
0 |
0 |
0 |
TUNDURU DC
|
0 |
0 |
0 |
0 |
MBINGA DC
|
1 |
250,000,000.00 |
4 |
390,000,000.00 |
SONGEA DC
|
0 |
0 |
4 |
240,000,000.00 |
NYASA DC
|
1 |
50,000,000.00 |
0 |
0 |
MADABA DC
|
1 |
50,000,000.00 |
0 |
0 |
MBINGA TC
|
0 |
0 |
0 |
0 |
NAMTUMBO DC
|
0 |
0 |
0 |
0 |
JUMLA
|
3 |
350,000,000.00 |
8 |
630,000,000.00 |
Miradi mingine inayotekelezwa
Jedwali Na 9: Miradi Mingine Inayotekelezwa na Halmashauri.
NA
|
HALMASHAURI
|
AINA YA MRADI
|
KIASI CHA FEDHA CHA MRADI
|
1 |
SONGEA MC |
Ujenzi wa Madarasa
|
227,250,000 |
Ukamilishaji wa mabweni 2
|
60,000,000 |
||
Ununuzi wa vifaa tiba katika zahanati
|
50,000,000 |
||
Ununuzi wa vifaa tiba katika vituo vya afya
|
150,000,000 |
||
Ukamilishaji wa ujenzi wa zahanati 1
|
50,000,000 |
||
Ujenzi wa hospitali ya wilaya awamu ya pili
|
500,000,000 |
||
JUMLA
|
1,037,250,000 |
||
2 |
TUNDURU DC |
Mfuko wa Jimbo
|
135,950,000.00 |
Ukarabati wa hospitali kongwe za halmashauri
|
900,000,000.00 |
||
Fedha za mitihani darasa la nne (SFNA 2022)
|
261,518,000.00 |
||
Fedha za Mitihani ya darasa la saba (PSLEE 2022)
|
120,042,000.00 |
||
fedha za mitihani kidato cha pili (FTNA 2022)
|
179,645,000.00 |
||
Fedha za Mitihani Kidato cha nne (CSEE 2022)
|
261,518,000.00 |
||
Elimu bure Shule za Msingi (EMBM)
|
335,913,531.39 |
||
Elimu bure shule za Sekondari (EMBM)
|
475,995,800.00 |
||
Tozo ya upandaji miti
|
44,012,084.50 |
||
Ununuzi wa vifaa tiba kwa zahanati
|
100,000,000.00 |
||
Ukamilishaji wa zahanati
|
200,000,000.00 |
||
Ununuzi wa vifaa tiba kwa vituo vya afya
|
300,000,000.00 |
||
Ujenzi wa madarasa shule kongwe za Msingi
|
100,000,000.00 |
||
Ukamilishaji wa madarasa msingi
|
100,000,000.00 |
||
Mfuko wa Jimbo
|
135,950,000.00 |
||
TASAF
|
1,778,703,691.00 |
||
UNICEF CHANJO
|
39,565,250.00 |
||
JUMLA
|
5,468,813,356.89
|
||
3 |
MBINGA DC |
EP4R
|
160,000,000 |
JUMLA
|
160,000,000.00 |
||
4 |
SONGEA DC |
Umaliziaji wa ujenzi wa zahanati za Magima na Mtimira B
|
100,000,000 |
Fedha za kuchochea miradi ya maendeleo (CDCF)
|
75,205,000 |
||
Ujenzi wa shule mpya ya Msingi lizaboni
|
250,000,000 |
||
Ukarabati shule ya msingi Liweta
|
100,000,000 |
||
Ujenzi Stand ya Mabasi kijiji cha parangu
|
225,145,486.29 |
||
Ujenzi nyumba ya Mtumishi na Kisima cha maji Zahanati ya mdunduwalo
|
170,995,797.32 |
||
JUMLA
|
921,346,283.61 |
||
5
|
NYASA DC
|
MAJENGO YA UTAWALA YANAYOENDELEA
|
448,402,504.81 |
6 |
MADABA DC |
Ukamilishaji wa Ujenzi wa Bwalo Shule Ya Sekondari Wino
|
50,000,000.00 |
Ukamilishaji wa Ujenzi Wa Bweni Shule Ya Sekondari Matetereka
|
80,000,000.00 |
||
Ujenzi wa Nyumba 4 za Walimu Shule Za Msingi (Mtazamo, Igawisenga, Madaba, Kifaguro)
|
200,000,000.00 |
||
Ukamilishaji wa Ujenzi wa Zahanati ya Mahanje
|
50,000,000.00 |
||
Ukamilishaji Wa Maabara 3 Katika Shule Za Sekondari (Madaba, Lilondo, Matetereka)
|
90,000,000.00 |
||
Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya
|
750,000,000.00 |
||
Ukamilishaji wa darasa 1 shule ya msingi Mbangamawe
|
18,750,000.00 |
||
|
|
JUMLA
|
1,238,750,000.00 |
7
|
MBINGA TC
|
0
|
0 |
8
|
NAMTUMBO DC
|
0
|
0 |
JUMLA
|
|
18,100,721,785.81
|
5.2.7 Baadhi ya Mafanikio ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya mwaka wa Fedha 2022/20223 kuishia Novemba, 2022
5.2.8 Changamoto za utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa mwaka 2022/2023.
5.2.9 Mikakati ya Kutatua Changamoto
Kununua vifaa vya ujenzi moja kwa moja viwandani ili kupata unafuu wa bei
Kupunguza matumizi yasiyo ya lazima
Kuendelea kuiomba Serikali kuridhia maombi ya kugawa maeneo ya kiutawala hususani Wilaya ya Tunduru pamoja na kuongeza fedha za uendeshaji wa shughuli za Mkoa na Halmashauri;
Kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa magari mapya na kufanya matengenezo ya magari yaliyopo.
Kuendelea kuwasilisha maombi ya vibali vya ajira ili kuongeza idadi ya watumishi na kuborehsa utoaji wa huduma mbalimbali.
5.3. Taarifa ya Maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024
Mkoa umeanza maandalizi ya mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa kuainisha vipaumbele mbalimbali vya kisekta kwa kuzingatia nyaraka na miongozo mbalimbali iliyopo ya kimkoa na kitaifa ili kuhakikisha Mpango na Bajeti ya Mkoa unaendana na vipaumbele vya kitaifa vilivyoainishwa katika Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 - 2025/26, Mpango wa II wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2021- 2025, Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 nk.
Sambamba na miongozo hiyo, Mpango na bajeti ya 2023/2024 utazingatia mwongozo wa Mpango na bajeti ya mwaka 2023/2024 uliotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango ambao unaainisha na kutoa maelekezo mahususi yanayopaswa kuzingatiwa na Wizara, Mashirika, Taasisi za Umma, Wakala za Serikali, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa wakati wa uandaaji wa Mipango na bajeti. Pamoja na kuzingatia vipaumbele vya Mwongozo wa mpango na bajeti, pia Mkoa utazingatia Vipaumbele vya Mkoa kama vilivyoainishwa katika Mpango Mkakati wa Mkoa wa miaka mitano (5) kuanzia 2021/2022 hadi 2025/2026, Mipango Mikakati ya Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi za Umma.
Baadhi ya Vipaumbele vya Mpango na Bajeti ya 2023/2024 ni kama ilivyoainishwa kwenye jedwali namba 10..
Jedwali Na 10: Vipaumbele vya Mkoa na Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2023/24
NA |
SEKTA |
VIPAUMBELE |
1.
|
Utawala na Rasilimali Watu
|
Kuendelea kusimamia na kudumisha masuala ya ulinzi na usalama ndani ya Mkoa pamoja na usimamizi wa mipaka kwa kuratibu vikao vya ujirani mwema.
Kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa kutenga fedha kwa ajili kujenga,kukamilisha na kukarabati nyumba na Ofisi za wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi wa Halmashauri,Tarafa, Kata na Vijiji na nyumba za watumishi kwa kuweka kipaumbele katika maeneo ambayo hayana ofisi na nyumba za viongozi na watumishi; |
2
|
Afya na Ustawi wa Jamii
|
Kuendelea kuboresha huduma za afya kwa kujenga, kukamilisha na kukarabati vituo vya kutolea huduma za afya na kuviwekea vifaa tiba na dawa.
Kuboresha huduma za afya na lishe katika ngazi ya jamii na vituo vya huduma za afya kwa kutenga bajeti ya uratibu, usimamizi na kujenga uwezo kuhusu masuala ya lishe sambamba na kutenga katika bajeti shilingi 1,000 kwa kila mtoto mwenye umri wa chini ya miaka mitano kwa ajili ya huduma za lishe. Kusimamia na kufuatilia ubora (Quality) na utoaji wa huduma za Afya katika Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati Kuendelea kutoa elimu ya kupambana na na kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa hatari ya kuambukiza ikiwemo ugonjwa wa Ebola, UVIKO 19, na Ukimwi. Kuendelea kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Jamii ulioboreshwa (iCHF). Kuwajengea uwezo watumishi wa Idara ya Afya katika vituo vya kutolea huduma za Afya katika Halmashauri. |
3.
|
Elimu na Mafunzo ya Ufundi
|
Kundelea kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia katika shule za msingi na sekondari kwa kujenga, kukamilisha na kukarabati miundombinu ya shule.
Kuendelea kutekeleza Mpango wa kutoa elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari ili kuwawezesha vijana wenye sifa kuanza na kuendelea na masomo bila kikwazo; Kuuwezesha mafunzo kazini kwa walimu katika ufundishaji wa mada mbalimbali. Kuboresha ufundishaji wa masomo ya sayansi na ufundi kwa kusambaza vifaa vya kufundishia masomo ya sayansi na kujenga maabara na karakana za ufundi. |
4
|
Kilimo na Mifugo
|
|
6
|
Nishati (Umeme)
|
Kuendelea na utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini na mijini inayotekelezwa na REA na TANESCO pamoja na kuendelea kuwaunganishia nishati ya umeme wananchi ili kuongeza kiwango cha upatikanaji wa umeme kwa ujumla (overall electricity access level)
|
7
|
Fedha na tehama
|
Kuendelea kuimarisha na kusimamia Mifumo ya Kielektroniki ya Ukusanyaji wa Mapato (LGRIS),mifumo ya matumizi (MUSE,FFARS etc) ili kupunguza mianya ya upotevu wa mapato ya serikali sambamba na kuendelea kuhimiza matumizi ya mifumo ya malipo Serikalini (GePG).
Kuendelea kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kubuni vyanzo vipya vya mapato na kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato katika vyanzo vilivyopo. |
9
|
Uwezeshaji wa wananchi kiuchumi
|
Kuendelea kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia utoaji wa mikopo yenye mashariti nafuu inayotokana na 10% ya mapato ya ndani ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu (4:4:2).
Kuendelea kusimamia na kutekeleza Mpango wa Kunusuru kaya Masikini (Social Welfare Benefits) unaotekelezwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF II). Kuendelea kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji mbalimbali kama viwanda, kilimo cha kimkakati, biashara nk. |
Kwa kuzingatia ukomo wa bajeti na vipaumbele vilivyoainishwa hapo juu, kwa mwaka wa fedha 2023/24 Mkoa wa Ruvuma fungu 82 unatarajia kuwasilisha maombi ya kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 267,530,798,000.00 kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake. Fedha hizo zinajumuisha Shilingi.180,932,942,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi. 86,497,856,000.00 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi na Shughuli mbalimbali za maendeleo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma na Halmashauri zake unatarajia kuwasilisha maombi ya kuidhinishiwa jumla ya Shilingi.180,932,942,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo,Shilingi. 153,907,956,000.00 ni Mishahara ya watumishi na Shilingi. 27,024,986,000.00 ni Matumizi Mengineyo. Aidha, bajeti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ni Shilingi. 6,419,485,740.00 na Shilingi.174,513,456,260.00 ni kwa ajili ya Halmashauri.
5.3.2 Matumizi ya Maendeleo
Kwa mwaka wa fedha 2023/24, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri zake unatarajia kuwasilisha maombi ya kuidhinishiwa makadirio ya jumla ya Shilingi. 86,497,856,000.00 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha hizo, Shilingi. 34,172,550,000.00 ni fedha za ndani, Shilingi. 45,511,358,000.00 ni fedha za nje na Fedha za maendeleo mapato ya ndani ni Shilingi 6,813,948,000.00. Fedha maendeleo kwa ajili ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ni Shilingi. 2,285,721,000.00 na Halmashauri ni Shilingi. 84,212,135,000.00.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.