WAZEE WA SONGEA WAKUMBUSHA AHADI YA KUREJESHA NCHINI KICHWA CHA SONGEA
WAZEE wa Baraza la Mila na Desturi la Mashujaa wa Majimaji la Songea wametoa rai kwa serikali kutekeleza ahadi walioitoa katika kumbukizi la miaka 113 ya mashujjaa wa vita ya Majimaji ya kurejesha nchini fuvu la kichwa cha Jemedari wa wangoni Nduna Songea Mbano kutoka nchini Ujerumani .
Jemedari wa wangoni Nduna Songea Mbano aliuawa na wajerumani mwaka 1906 pamoja na mashujaa wengine 66 wa vita ya Majimaji iliyopiganwa kuanzia mwaka 1905 hadi 1907.
Nduna Songea Mbano alizikwa kiwiliwili kwenye makaburi ya mashujaa wa vita ya Majimaji yaliyopo kwenye Makumbusho ya Taifa ya Majimaji mjini Songea ambapo kichwa chake kilikatwa na wajerumani na kwenda kuhifadhiwa nchini Ujerumani .
Katika kumbukizi ya miaka 113 mashujaa wa Majimaji serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii iliahidi kurejesha nchini fuvu la Nduna Songea Mbano pamoja na mafuvu mengine 200 ya mashujaa yaliyopo nchini Ujerumani ili kurejeshwa nchini na kufanyiwa maziko ya heshima.
Ifikapo Februari 27,2023 Mkoa wa Ruvuma utakuwa unafanya kumbukizi ya miaka117 ya mashujaa 67 wa vita ya Majimaji waliouwa kwa kunyonngwa na wajerumani Februari 27,1906.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.