• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

ASKOFU aipongeza serikali kwa kusimamia zoezi la sensa

Imewekwa kuanzia tarehe: August 30th, 2022

WANANCHI wa kata ya Matemanga wilayani Tunduru,wamewaomba makarani waliopewa  kazi katika zoezi la sensa ya watu na makazi,kuharakisha kuuliza maswali na kuchukua taarifa za kaya ili  kutoa fursa kwa wananchi kuendelea na shughuli za uzalishaji mali badala ya kukaa muda mrefu majumbani.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema,licha ya zoezi hilo kupokelewa vizuri lakini changamoto kubwa  ni makarani ambao wanatumia muda mrefu kufanya mahojiano na  kujaza taarifa za kaya,hivyo kusababisha baadhi  yao kushindwa kusubiri.

Askofu wa kanisa  la Upendo  wa Kristo Masihi  (Kiuma)wilayani humo Noel Mbawala alisema,muda wanaotumia makarani kujaza taarifa ya kaya moja kwenye vishikwambi ni mrefu ambapo ameshauri makarani hao kuongeza kasi ili  kuwafikia watu wengi kwa muda mfupi.

Alisema kutokana na majukumu ya wananchi  katika kujitafutia ridhiki,ni vyema makarani wakaongeza bidii ya kazi ili  watu wapate muda wa kwenda kwenye shughuli zao za kiuchumi na sio kukaa muda mrefu wakisubiri kuhesabiwa.

“zoezi hili la sensa linalofanyika ni zuri sana kwa maslahi ya nchi na taasisi  yetu ya Kiuma,hata hivyo tunawaomba  sana makarani waongeze spidi ya kujaza taarifa wanapofika kwenye kaya”alisema Askofu Mbawala.

Aidha,ameipongeza Serikali kwa  kuratibu vyema zoezi hilo kwani linatekelezwa kisasa ikilinganishwa na sensa zilizopita na litatoa fursa kwa serikali yetu  kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo.

Hata hivyo alisema,zoezi la sensa la mwaka huu liko tofauti na miaka ya nyuma kwani maswali  mengi yanayoulizwa  na makarani yanalenga kutatua changamoto za wananchi katika maeneo yao.

Askofu Mbawala,ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwani tangu ilipoingia madarakani imefanikiwa kutekeleza na kusimamia miradi  mingi ya maendeleo  katika maeneo mbalimbali hali iliyowezesha wananchi  kujikita katika kazi za kujiongezea kipato badala ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za kijamii mbali na makazi yao.

Hawa Athuman mkazi wa Milonde, alitaja changamoto ya zoezi hilo ni muda mrefu unaotumika kufanya mahojiano kwenye kaya moja yenye idadi kubwa ya watu na maswali yanayoulizwa na makarani ni mengi.

Fulko Hyera,amefurahishwa na  hatua ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuandaa zoezi la sensa  kwa mwaka 2022.

Alisema,wananchi wana matumaini makubwa kwa serikali yao kwani baada ya kupata takwimu na idadi sahihi ya watu  itaboresha huduma mbalimbali za kijamii kwa baadhi ya maeneo hapa nchini.

“baada ya zoezi hili,sasa serikali inaweza kujua kwa idadi ya watu waliopo wanahitaji maji kiasi gani,pembejeo za kilimo kiasi gani na huduma nyingine za kijamii ambazo zitatolewa kulingana na idadi ya wananchi wa eneo husika”alisema Hyera.Kwa upande wake Afisa wa sensa kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu anayesimamia tarafa ya Matemanga Nassoro Shamte alisema, kwa ujumla zoezi hilo linakwenda vizuri kutokana na hamasa kubwa  iliyofanywa na viongozi wa ngazi mbalimbali.

Alieleza kuwa, zoezi la sensa  katika tarafa ya Matemanga linaenda vizuri kutokana na idadi kubwa ya  watu kuelimishwa na wao kufahamu  kuhusu umuhimu wa zoezi hilo ambalo linafanyika kila baada ya miaka kumi hapa nchini.

Akizungumzia kuhusu changamoto hiyo Shamte alisema,viongozi  na makarani wamejipanga vizuri ili kuhakikisha kila mwananchi anahesabiwa na kuwatoa hofu wale ambao hawajahesabiwa  kuwa makarani watawafikia katika makazi yao.

Naye karani wa sensa Isaya Kalaliche alieleza kuwa,zoezi hilo limekuwa rahisi kwao kutokana na ushirikiano wanaoupata kutoka kwa viongozi wa vitongoji waliopo kwenye maeneo waliyopangiwa kwa ajili ya kuhesabu watu.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.