Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea Mhashamu Damian Denis Dallu amekemea uwepo kwa ndoa za jinsia moja na kuiomba jamii kukemea vitendo hivyo kwa nguvu zake zote.
Akiongea na waumini wa kanisa katoliki katika kanisa kuu la Mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba mjini Songea wakati wa kutoa shukrani kwa waumini kwa ukarimu wao kwa kanisa Askofu Dallu aliwataka waumini hao kusimamia maadili katika familia zao.
Dallu Aliwahimiza wazazi na walezi kutimiza majukumu yao ya kuwalea watoto katika malezi bora.
“Leo ni dominika ya mchungaji mwema ,tunaombea miito mitakatifu ili tupate watawa,mapadre,makatekista na ndoa, na chimbuka la kupata hayo ni kuwa na familia bora” alisema askofu huyo.
Dallu aliwaambia waumini hao kuwa mambo ya uhamasishaji kuhusu kuwepo kwa ndoa za jinsia moja zinapitia katika wizara ya afya na wizara ya elimu.
Telesphor Mbawala muumini wa kanisa katoliki alimpongeza Askofu Dallu kwa kuwahimiza waumini kuwa na familia zinazolelewa kwa kufuata maadili yaliyomema na waweze kuupinga ushoga kwa nguvu zao zote.
Dominika ya mchungaji mwema ni dominika ya kuombea miito mitakatifu katika kanisa katoliki hivyo waumini wamehimizwa kupinga ndoa za jinsia moja ili kuendelea kupata miito mitakatifu kwa kuwa na familia bora zenye maadili mema yenye kumpendeza Mungu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.