VIJIJI vinavyopata umeme katika Mkoa wa Ruvuma vimeongezeka kutoka vijiji 489 mwezi Machi 2024 Hadi kufikia vijiji 538 mwezi Mei 2024.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ruvuma Eliseus Mhelela amesema ongezeko hilo linatokana na kazi zinazofanywa na wakandarasi walioko katika vijiji mbalimbali mkoani Ruvuma.
Mhelela amesema mpaka kufikia Machi 2024 vijiji vilivyopata umeme vilikuwa 489 sawa na asilimia.88.3 ya vijiji vyote 554 vya Mkoa wa Ruvuma na kwamba katika kipindi hicho vijiji 65 tu vilikuwa havina umeme.
“Mpaka kufikia Mei 2024 vijiji vilivyopata umeme vimeongezeka kutoka 489 mwezi Machi 2024 mpaka kufikia vijiji 538 mwezi Mei 2024 sawa na asilimia 97.1”’alisema Mhelela.
Naye Mhandisi wa TANESCO Mkoa wa Ruvuma Malibe Boniphace amevitaja vijiji 16 tu katika Mkoa ambavyo bado havipata huduma ya umeme.
Hata hivyo amesema wakandarasi wanaendelea na kazi ya kusambaza huduma ya umeme katika vijiji hivyo vilivyobaki.
Boniphace ameyataja wateja ambao wananufaika kupitia mradi wa REA tatu mzunguko wa pili katika Mkoa wa Ruvuma kuwa ni wateja 5214.
Mkoa wa Ruvuma una jumla ya vijiji 554 na kati ya vijiji hivyo Tanesco imefanikiwa kufikisha huduma ya umeme katika vijiji 538 na kubakiwa na vijiji 16 Pekee..
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.