• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

BARABARA ya Mbinga-Mbambabay kufungua fursa mpya za kiuchumi Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: January 12th, 2021

Barabara ya Mbinga-Mbambabay kufungua fursa mpya za kiuchumi Ruvuma

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema kukamilika kwa ujenzi wa kiwango cha lami kwa barabara ya Mbinga hadi Mbambabay  yenye urefu wa kilometa 66 kunafungua fursa mpya za kiuchumi.

Mndeme alikuwa anazungumza wakati anafungua kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Ruvuma kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea mjini Songea.

“Niwahakikishie wananchi kuwa serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe.Dkt John Magufuli imedhamiria kukamilisha na kuunganisha maeneo mbalimbali ya Mkoa wetu kwa barabara za lami’’,alisema Mndeme.

Amesema barabara hiyo inafungua sekta ya usafiri na usafirishaji ukanda wa ziwa Nyasa hivyo kuhitimisha malengo ya serikali ya kufungua ushoroba wa Mtwara(Mtwara Corridor) na kuunganisha kwa urahisi na usafiri wa ndege kupitia kiwanja cha Ndege Songea na meli kupitia bandari ya Mbambabay ziwa Nyasa.

Mndeme amesisitiza kuwa kukamilika kwa mtandao wa barabara ya Mbambabay kumewezesha Mkoa wa Ruvuma kufunguka ambapo hivi sasa ajira na biashara zitaongezeka na kwamba hadi kufikia Desemba 2020,Mkoa ulikuwa na kilometa 9,321.38 za mtandao wa barabara.

Hata hivyo amesema kati ya kilometa hizo,Wakala wa Barabara Mkoa(TANROASDS)  anahudumia na kutunza  barabara zenye urefu wa kilometa 2,175.18.

Kwa upande wake Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Lazack Alinanuswe amezitaja barabara za Mkoa kuwa zina urefu wa kilometa 1,270.78 na  barabara kuu zina urefu wa kilometa 925.10.

“Wakala wa barabara za vijijini na mijini TARURA wanahudumia barabara zenye urefu wa kilometa 7,146.2,hadi sasa Mkoa umefanikiwa kuongeza mtandao wa kilometa 800.48 sawa na asilimia 8.6 ya barabara zote za TANROADS na TARURA’’,alisema.

Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa nchini ambayo makao makuu ya wilaya zote yameunganishwa kwa mtandao wa barabara ya lami.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Januari 11,2021

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.