WAZIRI wa Ujenzi Mheshimiwa Innocent Bashungwa ameeleza kuwa Serikali inatarajia kuanza kujenga upya barabara ya Songea – Njombe - Makambako kwa kiwango cha lami kutokana na barabara hiyo kuwa nyembamba na muda wake kuisha.
Bashungwa amesema hayo wakati wakati anazungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya za Mbinga,Nyasa na Songea kwenye mikutano ya hadhara akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Ruvuma.
Waziri Bashungwa ameeleza mikakati ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kufungua mikoa na nchi jirani kwa barabara za lami.
Bashungwa amesema hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu Serikali itakuwa imempata Mkandarasi atakayenga upya barabara Songea -Njombe ikiwa ni dhamira ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kufungua mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
“Ukitoka bandari ya Mtwara unakuja kwa lami hadi Songea, na kutoka Songea kwenda Njombe mjini kwenda makambako, lami ilijengwa miaka ya 80 imechoka, tayari Mheshimiwa Rais ametupatia fedha na kufika mwezi Machi au Aprili tutakuwa tumepata Mkandarasi ili kuijenga upya”, alisisitiza Bashungwa.
Bashungwa amewataka wananchi kuendelea kuheshimu Sheria na kutofanya shughuli katika maeneo ya hifadhi ya barabara ili kuondokana na usumbufu pale Serikali inapotumia Sheria zilizowekwa kuwaondoa katika maeneo ili kujenga miundombinu ya barabara
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.