Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Rajabu Mtiula amewatahadharisha waliokuwa Madiwani kuacha kujishughulisha na kazi za Udiwani baada ya muda wao kufikia ukomo.
Mtiula ametoa tahadhari hiyo Katika kikao Maalumu cha kuvunja Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo katika mji mdogo wa Peramiho.
“Baada ya leo kuvunja Baraza hili Madiwani hampaswi kujishughulisha na kazi zozote zinazohusiana na udiwani katika kata zenu kwa sababu utakuwa umevunja sheria na unaweza kushitakiwa’’,alisisitiza.
Hata hivyo Mtiula amemshukuru Mkurugenzi na Wataalamu wa Halmashauri hiyo kwa kazi nzuri ya kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kipindi cha miaka mitano.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Simoni Bulenganija amewashakuru madiwani hao kwa ushirikiano mkubwa waliotoa katika kusimamia shughuli mbalimbali za Halmashauri hiyo na kufanikiwa kutekeleza miradi mingi ya maendeleo kwa asilimia 100.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Menasi Komba akizungumza kwa niaba ya Madiwani ametoa rai kwa Wataalamu kuendelea kushirikiana ili kuwahudumia wananchi wa Halmashauri hiyo ambao wana kiu ya kupata maendeleo.
Kulingana na sheria,kanuni,taratibu na miongozo ya TAMISEMI ,ukomo wa kazi ya madiwani ni wa miaka mitano.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.