Sikukuu ya wakulima maarufu kama MAONESHO YA NANE NANE yaliyoanza tarehe 1 Agosti Songea Mkoani Ruvuma yamepambwa na Zao la Beetroots ambao umeonekana kuwa ni zao geni kwa wananchi wa Mkoa huo.
Akizungumza katika maonesho hayo ya Nane nane mtaalamu anayewakilisha mkoa wa Ruvuma na Njombe kutoka kampuni ya SEEDCO Frola Mgangala amesema Beetroots ni jamii ya kiazi chekundu na kwamba ni zao zuri katika kujenga afya ya binadamu akiwa mzima au mgonjwa.
‘’Beetroots ni mmea ambao unaongeza uwingi wa damu kwa saa 24,kwa wazee inaboresha cd4 zao, kwa sababu mwili unakuwa unashambuliwa na maradhi, inarudisha kinga vizuri,kwa akinamama wajazito wanapoenda kliniki wanapewa dawa badala yake wanaweza kutumia Beetroot,pia kwa watoto wadogo badala ya kutumia vitamini ‘’A’’ anaweza kutumia beetroot’,alisisitiza Mgangala.
Mtaalamu huyo wa SEEDCO ameelezea mmea wa Beetroot unaweza kumsaidia mgonjwa yeyote akiugua na kurudisha kinga ya mwili kwa haraka na majani ya mmea huo unaweza kutumika kama mboga zingine za majani,pia unaweza kutengeneza juisi na kuliwa kama karoti na kutumika kama kiungo cha mboga.
Afisa Kilimo kutoka Wilaya ya Tunduru Lucy Komba akizungumza kwenye maonesho hayo mjini Songea ameeleza kuwa mmea wa Beetroot unaweza kutumika kwa matumizi mengi hasa katika kuboresha afya ya binadamu.
‘’Matumizi ya mmea huo unaweza kutafuna kama kiazi au karoti inasaidia kwa wenye matatizo ya figo,kisukari,Ugonjwa wa moyo na kansa ’’,alisisitiza.
Hata hivyo Komba amesema zao hilo linaweza kulimwa kwenye bustani ndogo nyumbani tangu kupanda mpaka kukomaa linachukua muda wa miezi miwili na kuwa tayari kwa matumizi na mbegu ya zao hilo zinapatikana kila Halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma.
Kaulimbiu ya maonesho ya nanenane mwaka huu inasema kwa maendeleo ya kilimo,mifugo na uvuvi chagua viongozi bora 2020.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Ofisi ya Habari Mkoa Ruvuma
Agosti 4,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.