• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

HALMASHAURI Ruvuma zaagizwa kutekeleza HOJA za CAG

Imewekwa kuanzia tarehe: June 20th, 2025

Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo, ametoa maelekezo muhimu kwa Halmashauri za Mbinga Mji, Mbinga Vijijini na Madaba ili kutekeleza hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na maagizo ya Kamati ya Bunge ya LAAC.

Makondo ametoa maagizo hayo kwa nyakati tofauti wakati akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, katika mabaraza ya kujadili hoja za CAG yaliyofanyika katika halmashauri hizo.

Maagizo hayo ni wakuu wa idara na vitengo kushiriki kikamilifu katika kuandaa majibu ya hoja na mpango kazi wa utekelezaji wa hoja za CAG, Menejimenti kuhakikisha taarifa za hesabu za mwisho wa mwaka zinaandaliwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya uhasibu vinavyotumika katika sekta ya umma.

Maagizo mengine ni Wakurugenzi wa Halmashauri kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya watumishi watakaobainika kusababisha hoja au hasara kutokana na uzembe, pia Menejimenti kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za fedha na manunuzi, ili kuzuia hoja zisizo za lazima.

Vilevile, ameagiza hoja zote za miaka ya nyuma na maagizo ya LAAC katika halmashauri hizo yashughulikiwe kikamilifu na kufungwa kabla au ifikapo tarehe 30 Septemba 2025.

Kwa mujibu wa ripoti ya CAG kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2024, Halmashauri ya Mji wa Mbinga ilikuwa na jumla ya hoja 26, kati ya hizo hoja 6 pekee ndizo zilizofungwa na 20 zikiendelea kufanyiwa kazi. Pia, kuna hoja 16 za miaka iliyopita pamoja na maagizo matatu ya LAAC ambayo bado hayajatekelezwa kikamilifu.

Halmashauri ya Wilaya ya Madaba nayo ilipokea hoja 27 ambapo 12 zimefungwa, 15 bado zinaendelea kufanyiwa kazi, huku 10 zikiwa ni za miaka ya nyuma na maagizo mawili ya LAAC bado hayajatekelezwa ipasavyo.

Katika mabaraza hayo, Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Nickolas Kilinga, amezipongeza Halmashauri hizo kwa kupata hati safi  akisisitiza kuimarisha mifumo ya ukaguzi na udhibiti wa ndani ili kuepuka kuendelea kuwa chanzo cha hoja mpya.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Komredi Oddo Mwisho, ameeleza kuwa wakaguzi wa ndani ni chujio muhimu katika kugundua mapungufu, hivyo amesisitiza Halmashauri hizo kutoa usaidizi wa kutosha kwa wakaguzi hao ili waweze kufika maeneo mbalimbali, kukagua kwa wakati, na kuchukua hatua zinazostahili ili kupunguza au kuondoa kabisa hoja zinazojitokeza katika taarifa za CAG.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • UJENZI wa barabara ya kihistoria Tanzania na Msumbiji kuunganishwa kwa lamii kupitia Songea

    June 21, 2025
  • MADABA yafunguka ,uwekezaji wa bilioni 20 waleta mapinduzi katika afya na elimu

    June 21, 2025
  • HALMASHAURI Ruvuma zaagizwa kutekeleza HOJA za CAG

    June 20, 2025
  • SHULE hii haipo Ruvuma,serikali yaonya wanaosambaza uzushi

    June 19, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.