• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MADABA yafunguka ,uwekezaji wa bilioni 20 waleta mapinduzi katika afya na elimu

Imewekwa kuanzia tarehe: June 21st, 2025

 Katika kipindi cha miaka minne tu, Halmashauri ya Wilaya ya Madaba iliyopo mkoani Ruvuma imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo kiasi cha kugeuka mfano wa kuigwa kitaifa, hasa katika sekta za elimu na afya.

 Mafanikio haya yanatokana na utekelezaji thabiti wa miradi ya kimkakati chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na wanahabari mjini Madaba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Mary Makondo, alisema kuwa kuanzia mwaka 2021 hadi 2025, halmashauri hiyo imetekeleza miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 20.7, miradi ambayo imeleta mageuzi makubwa ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi.

MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA ELIMU YA MSINGI NA AWALI

Katika sekta ya elimu ya awali na msingi, ujenzi wa madarasa 68 mapya na ukarabati wa madarasa 25 umetatua changamoto ya msongamano wa wanafunzi darasani.

Aidha, ujenzi wa vyoo 257, nyumba nne za walimu na bweni moja umeongeza ustawi wa mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Pamoja na hayo, madawati 4,426 yamesambazwa katika shule mbalimbali, na hatua ya kujenga Kituo cha Rasilimali kwa Walimu inatajwa kuwa ya kimkakati kwani inalenga kuimarisha uwezo wa walimu kwa njia ya mafunzo endelevu.

"Tulikuwa na changamoto ya madarasa machache, lakini sasa watoto wanakaa kwa nafasi, wanajifunza vizuri, na hata ufaulu umeongezeka. Huu ni ushahidi wa dhamira ya kweli ya Rais wetu kwa elimu.",anasema mwalimu Grace Ngalema wa shule ya msingi Lituta Madaba.

SEKTA YA SEKONDARI YAPAA

Sekta ya sekondari haijabaki nyuma. Madarasa 53 mapya, vyoo 46 na nyumba 13 za walimu zimejengwa. Viti na meza 3,820 vimesambazwa kwa wanafunzi huku shule mbili zikiboresha miundombinu na kuanza kutoa elimu ya kidato cha tano na sita. Maabara 14 zimekamilika na moja kukarabatiwa, hatua inayosaidia kukuza elimu ya sayansi.

Shule mpya nne zimeanzishwa sambamba na ujenzi wa mabweni manne, bweni moja kukarabatiwa, na ukumbi wa chakula kujengwa.

Haya ni mafanikio yanayoongeza upatikanaji wa elimu bora kwa vijana wa Madaba, na kuvutia wanafunzi kutoka maeneo ya jirani.


"Mtoto wangu sasa anasoma sekondari yenye maabara na walimu wanaoishi karibu. Haya mambo yalikuwa kama ndoto miaka michache iliyopita.",anasema Rehema Kapinga Mkazi wa Lilondo

MABORESHO YA KUSISIMUA KATIKA AFYA

Katika sekta ya afya, awamu ya tatu ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Madaba imekamilika, ikijumuisha wodi ya upasuaji na barabara ya ndani yenye urefu wa mita 600.

Huduma za afya zimeimarishwa kwa kujengwa kwa kituo kimoja cha afya na zahanati nne mpya, hatua ambayo imepunguza umbali wa wananchi kutafuta matibabu.

Pia, vifaa vya nishati ya jua vimenunuliwa kwa vituo vya afya ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma wakati wote. Serikali imeongeza watumishi wa afya huku magari mawili ya wagonjwa na pikipiki nane zikinunuliwa kwa ajili ya huduma ya afya ya jamii, hasa maeneo ya pembezoni.


"Tumeweza kuongeza huduma za upasuaji, mama wajawazito hawasafirishwi tena kwa umbali mrefu. Tunaweza kuhudumia kesi za dharura hapa hapa Madaba."Anasema mmoja wa madaktari wa hospitali ya Madaba.

MATOKEO CHANYA YANAONEKANA

Mabadiliko haya yameleta matokeo chanya yanayoonekana. Uandikishaji wa wanafunzi umeongezeka, kiwango cha ufaulu kimepanda, na huduma za afya zimeimarika kwa kiasi kikubwa.

 Wananchi sasa wanapata huduma kwa wakati na kwa ubora, hali inayowajengea imani kubwa kwa Serikali yao.

Takwimu za Halmashauri zinaonesha kuwa zaidi ya watoto 8,000 wamefaidika na uboreshaji wa miundombinu ya elimu, huku zaidi ya wananchi 70,000 wakipata huduma bora za afya ndani ya kipindi cha miaka minne.

 wazi kwamba mafanikio ya Halmashauri  ya Madaba si ya kubahatisha, bali ni matokeo ya usimamizi madhubuti wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • UJENZI wa barabara ya kihistoria Tanzania na Msumbiji kuunganishwa kwa lamii kupitia Songea

    June 21, 2025
  • MADABA yafunguka ,uwekezaji wa bilioni 20 waleta mapinduzi katika afya na elimu

    June 21, 2025
  • HALMASHAURI Ruvuma zaagizwa kutekeleza HOJA za CAG

    June 20, 2025
  • SHULE hii haipo Ruvuma,serikali yaonya wanaosambaza uzushi

    June 19, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.