Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatekeleza mradi wa shilingi bilioni 14.56 wa kusambaza umeme katika vitongoji 135 Mkoani Ruvuma utakaonufaisha Kaya 4,455.
Mhandisi Msimamizi wa Miradi ya Umeme REA Kanda ya Kusini, Mhandisi Deogratius Nagu amebainisha hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Ahmed wakati wa kumtambulisha Mkandarasi aliyeshinda zabuni ya kutekeleza mradi huo Kampuni ya CCC International Nigeria LTD.
“Katika kuhakikisha maendeleo yanafika kote nchini, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeidhinisha kiasi cha shilingi bilioni 14.56 kitumike kutekeleza mradi wa kusambaza umeme katika vitongoji 135 Mkoani Ruvuma,” alisema Mhandisi Nagu.
Akizungumza wakati wa utambulisho wa Mkandarasi huyo, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Ahmed ameipongeza REA kwa kuendelea kutekeleza dhamira ya Rais Dkt. Samia kwa vitendo na amesisitiza Mkandarasi huo kuhakikisha anakamilisha mradi kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Mkoa wa Ruvuma una vitongoji 3,693 kati ya hivyo , vitongoji 1,973 vimefikishiwa umeme ambayo ni sawa na asilimia 53 na kwamba vitongoji 135 vitapata umeme kupitia mradi huo. unaotekelezwa katika majimbo tisa mkoani Ruvuma.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.