WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(RUWASA)wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma,umeanza kutekeleza mradi wa maji ya bomba wa Kitula kata ya Kitula Halmashauri ya wilaya Mbinga utakaowaondolea wananchi wa kata hiyo kero ya kuamka usiku wa manane na kutembea umbali mrefu kila siku kwenda kutafuta maji na kuacha shughuli za kujipatia kipato.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Mbinga Mhandisi Mashaka Sinkala amesema,mradi wa maji Kitula unatekelezwa kwa gharama ya Sh.bilioni 1.7 na utawanufaisha wananchi 9,100 wa vijiji vinne vya Mzuzu,Kitula,Mahilo na Lisau na utekelezaji wake umefikia zaidi ya asilimia 85.
Sinkala ametaja kazi zinazofanyika katika mradi huo ni ujenzi wa matenki matatu moja la lita 150,000 la pili la ujazo wa lita 100,000 la tatu lina uwezo wa kuhifadhi lita 75,000 na kulaza mabomba urefu kilometa 54.
Amesema, kazi zilizotekelezwa ni ujenzi wa matenki yote matatu na kujenga chanzo cha maji(Intake) na maji yameanza kufika kwenye matenki mawili kati ya matenki matatu kutoka kwenye chanzo.
Diwani wa Kata ya Kitula Mheshimiwa Alex Ngui amesema,mradi huo umewasaidia sana wananchi wa kata hiyo kupata huduma ya maji safi na salama kwenye maeneo yao na hivyo kupata muda mwingi wa kushiriki kazi mbalimbali za maendeleo.
Ngui amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi huo kwa kuwa utaleta tija kubwa kwa wananchi na kuharakisha maendeleo ya mtu mmoja mmoja,wilaya ya Mbinga na mkoa wa Ruvuma hasa ikizingatia kuwa wananchi wa kata hiyo ni wakulima wakubwa wa zao la kahawa linalohitaji maji mengi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.