Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi. Silvester Chinengo, amesema kiasi cha fedha Bilioni 21, 186, 188, 485 kimetegwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kwa ajili ya matengenezo ya barabara katika Wilaya ya Mbinga.
Amesema hayo wakati wa hafla ya makabidhiano ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Utiri -Mahande kwa kiwango cha lami kwa Mkandarasi Ovans Construction Limited iliyofanyika katika Kata ya Utiri Wilayani Mbinga.
"Bajeti ya Halmashauri ya Mji wa Mbinga inaonesha kuwa Bilioni 2, 348,450,000 zimetengwa na Serikali kwa ajili ya matengenezo ya barabara ambapo Milioni 848,450,000 zimetengwa kwa miradi ya ukarabati wa barabara, makaravati na madaraja, usimamizi na utawala, na Milioni 1,500,000 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo," alisema Mhandisi Chinengo.
Ameongeza kuwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Bilioni 2,637,500,000 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo ya barabara, ambapo Milioni 787, 500,000 zimetengwa kwa miradi ya ukarabati wa barabara, makaravati na madaraja, usimamizi na utawala, huku Milioni 1,850,000 zikitengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Mha. Chinengo amebainisha kuwa kupitia mradi wa Agriconnect unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya, Wilaya ya Mbinga imeidhinishiwa kiasi cha Bilioni 16,200,238,485 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Utiri -Mahande yenye urefu wa kilomita 14.414 hivyo kufanya bajeti ya Wilaya ya Mbinga kuwa jumla ya Bilioni 21,186,188,485 kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Kupitia mfuko wa Agriconnect unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya, TARURA imepanga kutekeleza mradi wa barabara ya Utiri-Mahande kwa kiwango cha lami na ufungaji wa taa za barabarani 107, kwa gharama ya Bilioni 16.2 chini ya Mkandarasi Ovans Construction Limited.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.