Serikali imetoa zaidi ya Sh.bilioni 4.45 kwa ajili ya kujenga shule ya Sekondari ya wasichana ya Mkoa wa Ruvuma yenye michepuo ya masomo ya Sayansi eneo la Migelegele wilayani Namtumbo.
Shule hiyo imesajiriwa kwa jina la Dkt Samia Suluhu Hassan ambapo hadi sasa ina wanafunzi 538 kati ya wanafunzi 610 waliopangiwa kusoma katika shule hiyo wakiwemo wa kidato cha kwanza(138)kidato cha tano(265) na wanafunzi wa kidato cha sita(210).
Mkuu wa shule hiyo Dafrosa Chilumba ametaja baadhi ya majengo yaliyokamilika kujengwa katika shule hiyo vyumba 22 vya madarasa maktaba,majengo ya TEHAMA,maabara nyumba za walimu,jengo la utawala na majengo mengine yanaendelea kujengwa na yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi.
Chlumba,amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi zilizowezesha kujengwa shule hiyo iliyotoa fursa kwa wasichana wengi wa mkoa wa Ruvuma na nchi kwa ujumla kupata nafasi kuendelea na masomo ya elimu ya juu.
“niseme tu ukweli katika shule hii kuna mazingira mazuri yanayomfanya mtoto kuwa na utulivu mkubwa na kusomo kwa bidii na walimu kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa,tunampongeza Rais Dkt Samia kwa kutuletea fedha za ujenzi wa shule yetu”alisema Chilumba.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.