Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma limeingia kwenye historia kwa kuzindua rasmi Bodi ya kwanza ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (TUUWASA)
,Tukio hilo limeelezwa kuwa ni hatua muhimu katika kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi. Bodi hiyo yenye wajumbe saba, imeundwa kwa mujibu wa miongozo ya kitaifa ya usimamizi wa maji katika miji midogo na makao makuu ya wilaya.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mheshimiwa Chacha, aliwataka wajumbe wa bodi hiyo kuhakikisha wanasimamia kwa weledi rasilimali za maji, miundombinu iliyopo, na kushirikiana kikamilifu na taasisi nyingine katika kutatua changamoto za huduma ya maji.
“Hali ya maji kwa sasa haitoshelezi mahitaji halisi ya wananchi. Maji ni uhai, na usimamizi wake unapaswa kuwa wa makini na wa kizalendo,” alisisitiza kwa msisitizo mkubwa.
Mheshimiwa Chacha alieleza kuwa wajibu mkubwa wa bodi hiyo ni kuhakikisha hakuna mwananchi anayekosa huduma hiyo muhimu kutokana na uzembe wa usimamizi. kuwa hatua za kimkakati zinahitajika ili kulinda vyanzo vya maji na kuhakikisha matumizi sahihi kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
“Tunapozungumzia maji, tunazungumzia maisha ya kila mmoja wetu,” alisema kwa msisitizo.
Katika hafla hiyo, Mhe. Chacha alimpongeza Mkurugenzi wa TUUWASA, Mhandisi Cuthbert Richard Kiwia, kwa uongozi bora usio na malalamiko, na kuahidi kuwa serikali itaendelea kuunga mkono mipango yote inayolenga kuboresha huduma hiyo. .
Bodi hii mpya inatarajiwa kuwa chachu ya mabadiliko makubwa katika sekta ya maji wilayani humo, huku Mhe. Chacha akihimiza wajumbe wake kuanzisha sheria ndogo ndogo zitakazosaidia katika utekelezaji wa majukumu yao
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.