Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mheshimiwa Jenista Mhagama ameagiza kuboreshwa Bwawa la maji la asili lililopo katika Kijiji cha Mpitimbi wilayani Songea mkoani Ruvuma ili liingizwe kwenye mpango ufugaji endelevu wa viumbemaji.
Waziri Mhagama amesema hayo wakati anazindua mradi wa kuimarisha lishe na ufugaji endelevu wa viumbemaji kwa wakulima wadogo uliofanyika Kijiji cha Mpitimbi wilayani Songea.
Katika mradi huo serikali kupitia shirika la IFAD imetenga kiasi cha shilingi bilioni 3.1 kutekeleza mradi huo katika wilaya za Songea na Mbinga mkoani Ruvuma na Wilaya za Ruangwa na Mtama mkoani Lindi,mradi ambao unatekelezwa kwa miaka miwili kuanzia Machi 2024 hadi Machi 2026.
“kuna bwawa la Mungu linalovutia sana lipo hapa Mpitimbi tena lipo njiani tu mnaweza kujionea ili kuangalia namna mnavyoweza kulitumia bwawa hilo la asili lenye ukubwa wa hekta 17 lenye uwezo wa kuingia samaki wengi kama litaboreshwa vizuri’’,alisisitiza Mhagama.
Mbunge huyo wa Peramiho amesema wamedhamiria kuiona Mpitimbi inakuwa kituo kikubwa cha ufugaji wa Samaki baada ya kuboresha bwawa hilo ambalo litakuwa kivutio kwa wawekezaji na chanzo kikubwa cha mapato na lishe bora kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma
Mhagama amesema Bwawa hilo ni kivutio kikubwa kwa wageni wengi pia linaweza kusaidia mradi huu wa ufugaji endelevu wa viumbemaji wakiwemo samaki ambapo Serikali ya Rais Samia imewekeza mabilioni ya fedha kutekeleza mradi huu.
Waziri Mhagama amebainisha kuwa wameanza kuteta na Mwakilishi wa Shirika la IFAD ili mradi wa bwawa la asili Mpitimbi uende sanjari na mradi wa shamba darasa la ufugaji Samaki lililopo Kijiji cha Mpitimbi
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.