Mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma, Ndg. Goas Mathei Mbawala amepongeza uwazi katika mchakato ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Namtumbo mwaka 2024,
kwa kutoa fursa kwa wagombea wa Vyama vyote vya Siasa kuingia katika kinyang'anyiro cha uchaguzi huo,
Pia amempongeza Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Ndg. Philemon Mwita Magesa kwa usimamizi mzuri wa Mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024,
Hata hiyo amesema inaonyesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kuweka usawa, haki na ukomavu wa kidemokrasia kwa Wilaya ya Namtumbo naTaifa kwa Ujumla.
Hata hivyo Mbawala amewataka wagombea Wengine wa vyama vya siasa kuhakikisha wanafuata vyema taratibu za kujaza fomu ili waweze kukidhi vigezo vya kugombea katika mihula inayofuta,
Pia ameshukuru wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi wilaya ya Namtumbo kwa kutenda haki katika mchakato mzima kuelekea katika zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 27 Novemba 2024.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.