Katibu Mkuu wa Chama cha Makini, Ameir Hassan Ameir, amepongeza uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika Novemba 27 mwaka huu, akisema ulikuwa huru na wa haki.
Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chama chao zilizopo kata ya Mjimwema mjini Songea.
“Tumesimamisha wagombea, na hakuna hata wakala mmoja aliyeleta ripoti kama kumetokea kasoro, kwa niaba ya chama Taifa, nikiwa kama Katibu Mkuu, naomba niseme kwamba uchaguzi huu wa Serikali za mitaa, vijiji pamoja na vitongoji ulikuwa huru na wa haki.” alisema Ameir.
Amekishukuru Chama cha Mapinduzi kwa kushirikiana na vyama vingine vyote kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa amani na utulivu kwani hata matokeo yaliyotangazwa ni wananchi walitumia haki yao ya kidemokrasia kuchagua viongozi wanaowataka.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Makini Tanzania bara, Grace Ngonyani, amewapongeza wananchi wote kwa kutumia haki yao ya kikatiba kwa kuwachagua viongozi watakaowaongoza katika mitaa, vijiji na vitongoji, pia, ameushukuru uongozi wa mkoa wa Ruvuma kwa ushirikiano mzuri walioupata katika ngazi zote walizopita.
Katibu wa Chama cha Makini Mkoa wa Ruvuma, Abdalla Ngonyani, amebainisha kuwa katika mkoa mzima wa Ruvuma, chama chao kilifanikiwa kuweka wagombea katika mitaa yote 123, kati ya vijiji 551 walifanikiwa kuweka wagombea katika vijiji 308 na kuweka wagombea katika vitongoji vyote 178.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.