• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

CHAMA Kikuu cha Ushirika Tunduru chavuka lengo uzalishaji wa korosho

Imewekwa kuanzia tarehe: February 22nd, 2022

WAKULIMA wa korosho mkoani Ruvuma wanaohudumiwa na Chama Kikuu cha Ushirika wilayani Tunduru(Tamcu Ltd), wamefanikiwa kuvuka lengo la uzalishaji kutoka kilo 24,000,000 msimu wa kilimo 2020/2021 hadi kufikia kilo 25,284,493 katika msimu 2021/2022.

Hayo yamesemwa jana na Meneja Mkuu wa Chama hicho Imani Kalembo, wakati akitoa taarifa ya uzalishaji na uuzaji wa korosho kupitia minada 13, katika kikao kazi cha mpango wa uchangiaji wa Pembejeo za wakulima kwa msimu wa kilimo 2022/2023.

Kalembo alisema, uzalishaji huo ni mafanikio makubwa tofauti na msimu wa mwaka 2020/2021 ambapo malengo yalikuwa kuzalisha kilo milioni 25, hata hivyo walizalisha kilo milioni 24.

Kwa mujibu wa Kalembo,mafanikio hayo yametokana na matumizi sahihi ya pembejeo ikiwamo Salphur,viuatilifu bora na wakulima kuzingatia maelekezo ya wataalam wa kilimo.

Kikao hicho kilichoongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Julius Mtatiro, kilihudhuriwa na Wenyeviti wa vyama vya msingi vya Ushirika(Amcos)Makalani na Wajumbe wa Chama Kikuu cha Ushirika Tamcu kilifanyika katika Ukumbi maarufu wa Klasta mjini Tunduru.

Kalembo, amewaeleza viongozi hao kwa niaba ya wakulima kuwa, utaratibu wa kuchangia pembejeo una faida nyingi ikiwamo uhakika wa kupata pembejeo kwa gharama nafuu ambapo mkulima atachangia asilimia 50 na Serikali itatoa asilimia 50.

Aidha alisema,utakomesha vitendo vya kitapeli kwa baadhi ya watu ambao kila msimu wanajipatia pembejeo hasa Sulphar bila kuwa na mashamba ya korosho na kwenda kuuza kwa wafanyabiashara kwa lengo la kujipatia fedha.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tamcu Mussa Manjaule amewahakikishia wanachama wa Amcos kuwa,mpango huo utaongeza uzalishaji wa zao la korosho katika msimu 2022/2023 kwa kuwa wakulima watakuwa na uhakika wa kupata pembejeo zilizo bora na kwa wakati na kuwaomba kuchangia kwa wingi ili wanufaike na punguzo la asilimia 50.


Manjaule ambaye ni mjumbe wa Bodi ya Korosho Tanzania,amewataka viongozi wa Amcos kwenda kuwashirikisha viongozi wa Serikali katika maeneo yao ili waweze kuwasaidia kufanikisha utekelezaji wa mpango huo badala ya kufanya kazi kwa kujificha.

Ameiomba Serikali kuwasaidia viongozi wa Amcos kutoa elimu kwa wakulima kuhusu umuhimu wa kuchangia pembejeo hizo,badala ya kuwaachia viongozi hao kwenda kuhamasisha mpango huo ambao unakusudia kuongeza uzalishaji wa korosho katika wilaya hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro, ametaja faida za kuchangia pembejeo kwa wakulima ni pamoja na kudhibiti biashara haramu ya viuatilifu inayofanywa na baadhi ya watu wachache na utasaidia viongozi wa Amcos kuwatambua wanachama wenye mashamba na wasio na mashamba.

Pia,ameagiza utaratibu wa kuchangia pembejeo kwa wakulima kuwa ajenda ya kudumu katika wilaya hiyo na elimu inatolewa kwenye mikutano mbalimbali ya vijiji na kata ambapo amewataka wataalam wa idara katika Halmashauri ya wilaya kuhakikisha kila wanapofanya mikutano ya maendeleo wanaeleza faida ya mpango huo.

Amewaasa viongozi wa vyama vya msingi, kufanya kazi kwa uaminifu,kufuata misingi na maadili katika utendaji wa kazi za kila siku na kuepuka vitendo vya wizi vinavyosababisha wanachama kutokuwa na imani kwa viongozi wao.

Aidha ametoa muda wa wiki moja kwa viongozi wa Amcos wilayani humo, kumaliza changamoto zilizopo kwenye vyama vyao kabla Serikali haijaanza kuchukua hatua dhidi yao na kuepuka kutafuta ugomvi na Serikali kwa kufanya mambo kinyume na sheria na taratibu zinazoongoza vyama vya ushirika.

Katika hatua nyingine Mtatiro alisema,mikakati madhubuti ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kutoa pembejeo na viuatilifu bure kwa wakulima umesaidia kuongeza uzalishaji wa korosho katika wilaya hiyo na mkoa wa Ruvuma.

Alisema, kwa mara ya kwanza wilaya ya Tunduru imefanikiwa kuingiza sokoni korosho zote daraja la kwanza na kuwataka viongozi wa Amcos kwenda kutoa elimu kwa wanachama juu ya kuzalisha korosho bora ambazo zitauzwa kwa bei ya juu ambayo itawanufaisha wakulima na kuwa na uhakika wa kupata fedha.

Amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan,kwa kuteua wasaidizi wazuri akiwamo Waziri wa kilimo Hussen Bashe ambaye ni mhimili mkubwa katika sekta ya kilimo hapa nchini ambapo kutokana na mikakati ya wizara ya kilimo,wilaya ya Tunduru ina matumaini makubwa ya kuendelea kuongoza katika uzalishaji wa zao la korosho Tanzania.
MWISHO.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.