Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa Ruvuma Ndugu Mohamed Ally amesema chama hicho kimedhamiria kuendeleza kampeni ya upandaji miti kwenye maadhimisho ya kuzaliwa CCM mwaka huu hiyyo amewaomba Wakala wa Misitu Tanzania TFS kuwaandalia miche ya kutosha ili kutekeleza mpango huo utakaosaidia kulinda na kuhifadhi mazingira ya Mkoa wa Ruvuma.
Mohomed ametoa ombi hilo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed wakati anazungumza kwenye uzinduzi wa upandaji miti ngazi ya Mkoa wa Ruvuma katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa,Songea ambapo Kanali Abbas amewaagiza TFS kuhakikjsha wanaandaa miche ya kutosha kufanikisha zoezi hilo ikiwa ni muendelezo wa kampeni za upandaji miti mkoani Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.