Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania kupitia Chama cha mapinduzi CCM Taifa Marry Chatanda, amewataka viongozi wa jumuiya hiyo kujikita katika kuwatumikia wananchi kwa kuangalia changamoto zao na kutatua.
Ameyasema hayo wakati anazungumza katika hafla ya kukabidhi mashine za kukamua alizeti na vyerehani pamoja na mitungi ya gesi kwa vikundi mbalimbali vya wanawake, iliyoandaliwa na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Ruvuma Mheshimiwa Jackline Msongozi vyenye thamani ya zaidi ya milioni 600.
Amewasisitiza wanawake hao kutunza mashine hizo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Amewasisitiza viongozi kuiga mfano wa Msongozi, katika kuangalia changamoto za wananchi wao na kuzitatua.
Chatanda pia amewaonya Wabunge na Madiwani wanawake ambao wanatabia ya kutoa pesa, kanga na rushwa nyinginezo ili kuwashawishi wajumbe wawape kura, badala yake amewataka kuwatumikia wananchi kwa haki .
Wakizungumza baadhi ya Wanavikundi waliopokea Mashine hizo pamoja na misaada mingine wamempongeza Mhe; Mbunge Msongozi kwa kuwapatia Mashine hizo ambazo zitaboresha maisha yao .
Mbunge Msongozi amekabidhi Mashine 20 za kukamua alizeti kwa Vikundi 20 zenye thamani ya milioni 400, cherehani 700 zenye thamani ya milioni 200 majiko ya gesi 500, ng'ombe wawili kwa familia zenye uhitaji mifuko ya simenti kwenye misikiti, makanisa na shule.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.