Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amekagua Daraja la Ruhuhu lenye urefu wa mita 98 ambalo linaunganisha Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma na Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe ambalo limekuwa mkombozi kwa wananchi wa Mikoa hiyo.
Ameongeza kuwa kukamilika kwa daraja hilo kumewafanya wananchi waishio nje ya mikoa ya Njombe na Ruvuma kupenda kuja kwao na kutumia usafiri wa magari kupitia daraja hilo.
“Niendelee kumshukuru Mhe. Rais kwa namna ambavyo anaendelea kufanya jitihada ya kuwaanganisha watanzania kwa miundombinu ya barabara kwa kiwango cha lami lakini hata zile za changarawe zinaendelea kuboreshwa”, amesisitiza Bashungwa.
Bashungwa amefafanua kuwa Daraja hilo ni moja ya ahadi na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), pia ni moja ya mkakati wa Serikali wa kuunganisha miundombinu ya barabara na madaraja katika mikoa na nchi jirani zinapopakana na nchi yetu ya Tanzania.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Ruvuma , Komred Oddo Mwisho, ameeleza kuwa hapo awali kabla Daraja hilo halijakamilika kulikuwa na changamoto mbalimbali ikiwepo wamama wajawazito kujifungulia nyumbani.
Naye, Mkazi wa Lihuli Bw. Michael Ngonyani, ameishukuru Serikali kwa kukamilisha ujenzi wa Daraja hilo kwani kumewarahisishia usafiri kutoka Mkoa wa Ruvuma kwenda Mkoani Njombe kupitia daraja hilo.
Vilevile ameiomba serikali kuweza kuwasaidia kuunganisha barabara za pande zote mbili kwa kiwango cha lami.
Utekelezaji wa mradi wa Daraja la Ruhuhu ulikamilika Disemba, 2021 na uligharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 8.9 ikiwa ni zote ni fedha za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.