Kikao cha lishe Bora kwa kipindi cha robo ya tatu kwa mwaka wa Fedha 2023/2024,kimefanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea uliopo Lundusi Peramiho.
Kimeazimia mikutano yote itakayofanyia kwenye Halmashauri hiyo kuhakikisha wanatoa elimu ya Lishe bora kwa wananchi.
Akizungumza kwenye kikao hicho Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Mtela Mwampamba amesisitiza kutolewa elimu ya lishe bora na ulaji unaofaa kwa jamii kupitia Mikutano yote ya Hadhara, Makongamano, Semina na vyombo vya Habari.
Katibu Tawala huyo amewasisitiza walimu wakuu wa Sekondari na Msingi, kuhakikisha wanalima bustani za mboga mboga kwenye maeneo yao ya shule ili kuwa na uhakika wa mboga za majaji kwa wanafunzi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.