Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mheshimiwa Aziza Mangosongo ametoa siku mbili kwa Kampuni za mikopo ya fedha kurudisha kadi za benki za watumishi kwa kuwa ni kinyume cha sheria kumiliki kadi za benki ambazo sio mali yao.
Mangosongo ametoa agizo hilo wakati anazungumza na wakuu wa Taasisi za kibenki,kampuni za ukopeshaji fedha na watumishi wa kada tofauti za elimu, afya, utawala katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa FDC mjini Mbinga.
“Ni kosa kisheria kumiliki kadi ya benki ambayo sio mali yako hata kama watumishi hao wanadaiwa “,alisema Mangosongo.
Amesema asilimia kubwa ya watumishi huacha kadi zao kwa wakopeshaji kama dhamana hali ambayo urahisisha miamala ya kifedha kufanyika muda wowote pasipo uangalizi wa wahusika.
Hata hivyo Mangosongo amezitaka kampuni hizo kuwasilisha nyaraka na taarifa za mikopo Kiwango cha riba kinachotozwa pamoja na changamoto zinazowakabili wakopeshaji na wakopaji.
Amemuagiza Afisa Biashara wa Halmashauri ya Mji Mbinga kukagua upya leseni za kampuni hizo ili kuona uhalali wake.
Mkuu wa Wilaya ametoa rai kwa watumishi kubuni miradi mipya ya kuwaingizia kipato nje ya kazi zao, ili kuepuka mikopo isiyo na tija
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Msingi Mihango Geofrey Rugomora amesema watumishi wengi ni wahanga wa mikopo hiyo lakini kutokana na elimu mpya ambayo wameipata itasaidia kuongeza umakini kabla ya kufanya maamuzi ya kukopa fedha hizo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.