Mkuu wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Mhe. Aziza Ally Mangosongo ameipongeza Kampuni ya uchimbaji Makaa ya Mawe Ruvuma Coal Limited kwa kwa kutekeleza mpango wa uwajibikaji kwa Jamii (CSR) hatua ambayo inaleta maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Mangosongo ametoa pongezi hizo katika hafla ya kukabidhi madawati 50 kati ya 270 pamoja na meza 5 za walimu Shule ya Msingi Paradiso iliyopo Kata ya Ruanda vifaa ambavyo vimetolewa na Kampuni hiyo ya uchimbaji..
Kwa upande wake Afisa Maendeleo kutoka Kampuni ya Ruvuma Coal Limited Bi. Aisha Hamis ameeleza kampuni hiyo imekuwa ikiwajibika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika vijiji viwili vinavyozunguka mgodi ambavyo ni Sara na Paradiso.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.