Maandalizi yanaendelea kwa uzinduzi wa Siku ya Mwanamke Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma , tukio linalotarajiwa kufanyika tarehe 6 Machi 2025 katika Gereza la Kitai.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Mhe. Kisare Makori.
Mbali na uzinduzi, Mhe. Makori ataungana na wanawake wa Wilaya ya Mbinga katika shughuli ya kukabidhi mahitaji muhimu kwa wafungwa wa gereza hilo, ikiwa ni ishara ya mshikamano na kuunga mkono ustawi wa jamii zote.
Wadau mbalimbali wanakaribishwa kushiriki kwenye hafla hiyo, ambayo inaenda sambamba na kauli mbiu ya mwaka huu: “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji!”
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.